
KRC GENK YA UBELGIJI, PYRAMIDS FC NA RS BERKANE ZAPIGANA VIKUMBO KUMSAJILI ELIE MPANZU
Taarifa tulizozipata kutoka kwenye chanzo chetu cha kuaminika zinaeleza kuwa kuna klabu tatu zinazomfuatilia kwa karibu kiungo mahiri Mpanzu, ambaye ameonesha kiwango bora kwenye mashindano ya CAF msimu uliopita.
Klabu hizo ni KRC Genk ya Ubelgiji, Pyramids FC ya Misri na RS Berkane ya Morocco. Kwa mujibu wa taarifa hizo, KRC Genk tayari wamejiridhisha na uwezo wa Mpanzu na wako tayari kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili.