
Bayern Munich inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27, baada ya kuvutiwa na kiwango cha mchezo wake akiwa Aston Villa kwa mkopo msimu uliopita. (Sun)
Arsenal inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres. Mchezaji huyo wa Uswidi aliye na umri wa miaka 27 ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na The Gunners. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Crystal Palace imefikia makubaliano ya pauni milioni 47 kumsajili Ousmane Diomande, 21, kutoka Sporting huku beki huyo wa Ivory Coast akionekana kama mbadala wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marc Guehi, 24. (A Bola - kwa Kireno)
Manchester United imewasiliana na Inter Milan kuhusu dili la kumsaini kiungo wa wa Italia Davide Frattesi, 25. (Caught Offside)Arsenal tayari imewasilisha ofa ya kumsajili winga wa Uingereza Noni Madueke, 23, ambaye huenda akaondoka Chelsea msimu wakiangazi. (Sky Germany)
End of Iliyosomwa zaidi
Juventus inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 25, ambaye mkataba wake na klabu ya Lille ilikamilika mwishoni mwa msimu uliopita. (Fabrizio Romano)
Mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 22, anaelekea Uturuki kukamilisha mchakato wa uhamisho wake wa bure kutoka Al-Nassr kwenda Fenerbahce. (Athletic-Usajili unahitajika)

Newcastle wanatafakari uwezekani wa kumsajili beki wa Marseille na Argentina Leonardo Balerdi, 26, ambaye pia anafuatiliwa na Juventus. (Mail- usajili unahitajika)
AC Milan ina matumaini ya kumsajili kiungo wa Uswizi Ardon Jashari, 22, kutoka Club Brugge kwa mkataba wa takriban £30m. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester City itamsajili kinda wa miaka 15 Caelan-Kole Cadamarteri kutoka Sheffield Wednesday kwa mkataba wa £1.5m. Cadamarteri ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Everton Danny. (Mail)