A Zeno.FM Station Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: West Ham yakataa ombi la Tottenham kumsajili Kudus

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: West Ham yakataa ombi la Tottenham kumsajili Kudus

 


Mohammed Kudus

Chanzo cha picha,Getty Images

West Ham imekataa dau la pauni milioni 50 iliyowasilishwa na Tottenham kumsajili mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 24. (Talksport)

Arsenal ina matumaini ya kumpata mshambuliaji wa Brazil Rodrygo kwa pauni milioni 70. Mchezaji huyo hana uhakika wa kusalia Real Madrid chini ya kocha mpya Xabi Alonso. (Mirror)

Atletico Madrid iko tayari kufanya kila iwezalo kumsajili beki wa Tottenham na Argentina Cristian Romero, 27, na iko tayari kufikia mkataba wa thamani ya takriban £61m. (AS - kwa Kihispania)

Manchester United inataka pauni milioni 25 kumuachilia Jadon Sancho, 25, huku Juventus ikiwa bado na nia ya kumsajili winga huyo wa Uingereza. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano

Sancho yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kujiunga na mabingwa hao wa ligi ya Serie A. (Eurosport Italia - kwa Kiitaliano)

Manchester United imepiga hatua katika mbio za kusajili mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, 29, na imefanya mazungumzo ya muda na klabu hiyo ya Midlands inayotaka ada ya takriban £60m. (Mirror)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Jadon Sancho

Mkufunzi wa Napoli Antonio Conte ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta msimu huu wa kiangazi. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Winga wa Japan Kaoru Mitoma, 28, ameiambia Brighton kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo na kusaini mkataba mpya licha ya kuhusishwa na kuhamia Bayern Munich (Sky Sports)

Kipa wa Nice Marcin Bulka, 25, anatarajiwa kujiunga na Neom ya Saudi Arabia, licha ya Sunderland kuwasilisha ofa ya pauni milioni 12.8 iliyokubaliwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland. (Meczyki - kwa Kipolandi)

Kauro

Chanzo cha picha,Getty Images

Mshambulizi wa Italia Ciro Immobile, 35, anatarajiwa kukatisha mkataba wake na klabu ya Uturuki ya Besiktas na kujiunga na Bologna kwa uhamisho wa bila malipo. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Beki wa Valencia Mhispania Cristhian Mosquera, 21, amekataa kandarasi mpya iliyoboreshwa na klabu hiyo ya La Liga kwa sababu anataka kujiunga na Arsenal. (Las Provincias - kwa Kihispania)

Beki wa Wolves Nasser Djiga, 22, huenda akajiunga na Rangers kwa mkopo kwa msimu huu akiwa amecheza mechi tano pekee za Ligi ya Premia tangu Februari. (Express na Star)

Tags :-

Post a Comment

0 Comments