A Zeno.FM Station Yanga Uwanja Tunao na Tunatamba Nao, Hersi Atoa Msimamo

Yanga Uwanja Tunao na Tunatamba Nao, Hersi Atoa Msimamo


Rais wa klabu ya Yanga Sc Hersi Said amefunguka mambo mazito kuhusiana na mchakato na mpango wa uongozi wake katika suala zima la kutekeleza mchakato wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo.

Ikumbukwe kwamba mpaka sasa Yanga Sc kama klabu kongwe nchini Tanzania haina uwanja wake wa kuchezea mechi za kimashindano kitu ambacho huwa kinaleta changamoto sana pindi uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam unapokuwa anafanyiwa matengenezo.

Hersi Said wakati anaingia madarakani miaka miwili iliyopita alitoa ahadi ya kujenga uwanja wa kisasa wa klabu hiyo katika awamu yake ya kwanza ya kukaa madarakani na sasa ameibuka hadharani kwa maana kwamba anataka kukamilisha mpango huo.

Hersi Said katika taarifa yake aliyoitoa siku ya jana Jumatatu tarehe 30 Juni, akiwa kwenye sherehe za ubingwa ambazo ziliandaliwa na klabu hiyo, aliwaeleza mashabiki na wadau wa klabu ya Yanga Sc kwamba miezi mitatu ijayo klabu itaanza ujenzi rasmi wa uwanja wao.

Hersi Said katika taarifa alieleza wazi kwamba mpaka sasa tayari serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan imeshatoa kibali cha Yanga Sc kujenga uwanja wao mitaa ya jangwani hivyo basi kwa sasa wanasubiriwa viongozi qa klabu hiyo walete wakandarasi ambao wameomba tenda ya kufanya ujenzi huo.

Hersi Said katika uongozi wake ni kama amekuwa na weledi mkubwa sana katika kuendesha mambo ya klabu hiyo na pengine ndio maana klabu imekuwa ikipata mafanikio makubwa kwenye michuano ya ndani pamoja na ile ya kimataifa.

Yanga Sc wanaongozwa na viongozi bora na wenye maono chanya na klabu hiyo ukilinganisha na viongozi wa vilabu vingine vinavyoshiriki Nbc Premier league.


Tags :-

Post a Comment

0 Comments