Yanga SC Kuanza Ujenzi wa Uwanja Wake Ndani ya Miezi 18
Yanga SC Yaingia Ubia na GSM Group Kujenga Uwanja wa Kisasa wa Kihistoria
0 (Yanga SC) imetangaza rasmi kuingia katika hatua mpya ya kihistoria ya ujenzi wa uwanja wake binafsi, ndoto ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa takribani miaka 90 ya historia ya klabu hiyo.
Akizungumza kuhusu mradi huo, 1 amesema uongozi na wanachama wa Yanga wanapaswa kujivunia juhudi za viongozi waliopita walioweka msingi imara wa klabu, ikiwemo kuhifadhi ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 35,000 kwa zaidi ya miaka 50.
Kwa mujibu wa Hersi, mafanikio ya Yanga ndani ya uwanja pamoja na ukuaji wa mapato na wanachama yameongeza mvuto kwa wawekezaji na kufungua milango ya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya klabu.
Baada ya mchakato wa zabuni, Kamati Kuu ya Yanga iliidhinisha 2 kuwa mbia mkuu wa mradi huo mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa kisasa.
3, ambaye ni Rais wa GSM Group, atashirikiana na Yanga SC katika ubia wa umiliki wa uwanja kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50.
Katika makubaliano hayo, Yanga SC itachangia ardhi huku GSM Group ikitoa mtaji wa kifedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo unaotarajiwa kubadilisha historia ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa uongozi wa klabu, ujenzi wa uwanja huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 20, na uzinduzi wake rasmi utaashiria mwanzo wa enzi mpya kwa Wananchi.
Mradi huo umetajwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi katika historia ya Yanga SC, ukiwa na lengo la kuimarisha hadhi ya klabu ndani na nje ya Tanzania.




No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.