Vanessa Kashera Afunguka Madai ya Ujauzito
Vanessa Kashera Afunguka Madai ya Kubeba Mimba ya Morice Abraham
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii, bila shaka utakutana na gumzo kuhusu muigizaji wa tamthilia Vanessa Kashera maarufu kama Vee, ambaye pia ni mzazi mwenza wa nyota wa zamani wa Yanga, Stephane Aziz KI.
Tetesi hizo zimeenea kwa kasi zikidai kuwa Vanessa ana ujauzito wa mchezaji wa Simba SC, Morice Abraham.
Baadhi ya watu kwenye mitandao wamekuwa wakihusisha madai hayo na sababu ya Aziz KI kuachana na Vanessa kabla ya mwanasoka huyo kuanza maisha mapya na Hamisa Mobetto.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi, Vanessa amesema ni kweli ana ujauzito na anatarajia kupata mtoto lakini si wa Morice Abraham kama inavyodaiwa na wengi mtandaoni.
Vanessa ameeleza kuwa Morice Abraham ni mtu wa karibu sana kwenye familia yao na hata humuita shemeji yake.
Pia amesisitiza kuwa taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye na Morice si za kweli.
Sakata hilo limeendelea kuzua mjadala mkubwa mtandaoni huku mashabiki wa mastaa hao wakitoa maoni tofauti kuhusu maisha binafsi ya watu maarufu.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za mastaa, burudani na gumzo za mitandaoni.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.