-->

Breaking News

Nandy Afunguka Maadhimisho ya Miaka 10 Kwenye Muziki Yatakavyokuwa

Nandy Afunguka Maadhimisho ya Miaka 10 Kwenye Muziki Yatakavyokuwa

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, amesema maadhimisho ya miaka 10 ya safari yake ya muziki mwaka huu yatakuwa tofauti na miaka iliyopita huku akiahidi burudani ya kipekee kwa mashabiki wake.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Juni 10, 2026 mkoani Shinyanga, ambapo maandalizi yanaendelea sambamba na mipango mingine ya kazi za msanii wake Pipijojotz.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Nandy alisema safari yake ya muziki imekuwa na mafanikio makubwa tangu alipoanza rasmi miaka 10 iliyopita.

Mbali na mafanikio hayo, Nandy amesema upinzani kwenye muziki umekuwa sehemu muhimu iliyomsaidia kukua zaidi kisanaa na kutoa kazi bora kwa mashabiki wake.

“Mimi ni mtu ambaye napenda sana upinzani, kwa sababu umenipa kitu kikubwa. Tuendelee kuchalenjiana kwani hiyo ndiyo inawapa mashabiki nafasi ya kupata kazi nzuri kutoka kwetu,” alisema Nandy.

Msanii huyo pia alisema muziki umemfungulia milango mingi ya biashara anayofanya pamoja na mume wake, Billnass.

“Biashara zetu nyingi zimetokana na muziki kwa sababu mashabiki wetu ndiyo wamekuwa wateja wetu wakubwa. Tunawashukuru sana kwa namna wanavyoendelea kutuunga mkono kila siku,” alisema.

Katika kipindi cha miaka 10 ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nandy ameendelea kuwa mmoja wa wasanii wanawake wenye mafanikio makubwa Tanzania kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za Bongo Fleva, mastaa wa Tanzania na burudani za Afrika Mashariki.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.