Rekodi 10 Kubwa Ambazo Diamond Platnumz Bado Anazishikilia Afrika
Rekodi 10 Kubwa Ambazo Diamond Platnumz Bado Anazishikilia Afrika
Diamond Platnumz ameendelea kuweka historia kubwa katika muziki wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kupitia mafanikio na rekodi mbalimbali ambazo bado hazijavunjwa mpaka sasa.
Kwa zaidi ya miaka 17 tangu aanze safari yake rasmi ya muziki, Diamond ameweza kujijengea heshima kubwa ndani na nje ya Afrika kupitia tuzo, mafanikio ya kidijitali na ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya burudani.
1. Msanii Aliyeshinda Tuzo Nyingi Zaidi za TMA
Diamond ndiye mwanamuziki aliyeshinda mara nyingi zaidi Tanzania Music Awards (TMA) akiwa na zaidi ya tuzo 22. Katika TMA 2024 alishinda vipengele vinne tofauti.
2. Rekodi ya Kushinda Tuzo 7 kwa Usiku Mmoja
Mwaka 2014 Diamond aliweka rekodi ya kushinda tuzo saba za TMA kwa usiku mmoja, rekodi ambayo bado haijavunjwa.
3. Msanii Mwenye Ushawishi Mkubwa Mitandaoni Afrika Mashariki
Diamond anaongoza kwa idadi ya wafuasi kwenye Instagram, Facebook, X, TikTok na YouTube katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
4. Mfalme wa AEAUSA
Diamond ndiye msanii wa Afrika Mashariki aliyeshinda tuzo nyingi zaidi za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) akiwa na tuzo nane.
5. Msanii Mwenye Subscribers Wengi YouTube Afrika
Diamond ana subscribers milioni 11.4 kwenye YouTube na ndiye msanii wa kwanza Afrika Mashariki kupata Diamond Creator Award baada ya kufikisha subscribers milioni 10.
6. Msanii wa Kwanza Afrika Mashariki Kuingia Billboard U.S Afrobeats
Wimbo wake wa Komasava uliingia kwenye chati ya Billboard U.S Afrobeats Songs, kitu ambacho hakuna msanii mwingine wa Afrika Mashariki aliyewahi kufanya.
7. Video Nyingi Zaidi Zenye Views Milioni 100+
Diamond ndiye msanii pekee Afrika Mashariki mwenye video sita zilizovuka views milioni 100 YouTube, zikiwemo Yope Remix, Inama, Waah!, Nana, Jeje na African Beauty.
8. Mastaa Wengine Wenye Video Milioni 100+
Baada ya Diamond, wasanii wengine kama Harmonize, Zuchu, Jux na Rayvanny wana video moja moja zilizofikisha views milioni 100.
9. Rekodi ya MTV Europe Music Awards
Diamond anaongoza Afrika kwa kushinda tuzo nyingi zaidi za MTV Europe Music Awards (EMAs), akiwa ameshinda tatu.
10. Rekodi Inayoendelea Kusimama Afrika
Licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa mastaa wa Afrika kama Tyla, Burna Boy na Wizkid, Diamond bado anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wenye rekodi nyingi zaidi barani Afrika.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za Diamond Platnumz, Bongo Flava na burudani za Afrika.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.