-->

Breaking News

Poshy Queen azawadiwa gari Land Cruiser 300

 

Poshy Queen akiwa na Land Cruiser 300 mpya Tanzania

Sosholaiti maarufu nchini Tanzania, Poshy Queen, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuweka wazi kuwa amenunuliwa gari jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser 300 na mpenzi wake anayemtaja kama “Daddy”.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Poshy Queen alionyesha furaha yake kubwa kwa zawadi hiyo ya thamani inayokadiriwa kufikia kati ya Sh300 milioni hadi Sh500 milioni.

Poshy Queen akiwa na Land Cruiser 300 mpya Tanzania

“Asante daddy 🥰😫 mwaka jana Aprili nilikuwa nasherehekea Range Rover yangu mpya, mwaka huu Aprili umeenda mbali zaidi – Land Cruiser 300 mpya kabisa ya 2025,” aliandika Poshy Queen.

Kauli hiyo iliambatana na ujumbe wa mapenzi uliovutia mashabiki wengi, huku akiweka wazi matarajio yake ya zawadi nyingine kubwa zaidi mwaka ujao.

“Natazamia Aprili ya mwaka ujao ❤️🥰. Nakupenda sanaaaa 😫❤️🙏🏽 Mungu akubariki sanaaaa 🙏🏽❤️,” aliongeza.

Tukio hilo limezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo baadhi ya mashabiki wameonyesha furaha na kumpongeza, huku wengine wakibaki na maswali kuhusu utambulisho wa “Daddy” huyo.

Ikumbukwe kuwa hapo awali Poshy Queen aliwahi kuwa kwenye uhusiano na msanii wa Bongo Fleva Harmonize, ambapo walidumu kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kuachana.

Poshy Queen akiwa na Land Cruiser 300 mpya Tanzania

Kwa sasa, Poshy Queen anaendelea kuwa mmoja wa mastaa wa mitandaoni wanaovuta attention kubwa kutokana na maisha yake ya kifahari, mahusiano yake, pamoja na mitindo yake ya maisha inayovutia wengi.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.