Diva Wasafi FM Afunguka Maisha Yake: “Nilikuwa Natumia Private Jet Utotoni”
Mtangazaji wa Wasafi FM, Diva, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kufunguka kuhusu maisha yake ya kifahari aliyoyaanza tangu utotoni.
Akizungumza katika kipindi cha Exclusive, Diva alieleza kuwa baba yake mzazi alikuwa na ndege binafsi (private jet), jambo lililomfanya kukulia katika mazingira ya hali ya juu tangu akiwa mdogo.
Kauli hiyo imekuja kufuatia madai ya baadhi ya watu kudhani kuwa anaigiza maisha ya kifahari. Hata hivyo, Diva alikanusha vikali akisema hana sababu ya kuigiza kwani maisha hayo ni sehemu ya historia yake halisi.
Aidha, alieleza kuwa wakazi wa Bukoba wanaweza kuthibitisha hilo, akidai kuwa alikuwa akichukuliwa kwa ndege mara kwa mara akiwa mdogo.
Mbali na hilo, Diva aliwahi pia kudai kuwa matumizi yake ya kila mwezi yanafikia zaidi ya Sh30 milioni, kauli iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni huku mashabiki wakitoa maoni tofauti kuhusu maisha yake.
Kwa sasa, Diva anaendelea kuwa miongoni mwa watangazaji wanaovuta attention kubwa nchini Tanzania kutokana na maisha yake, kauli zake, pamoja na uwepo wake kwenye media.



No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.