-->

Breaking News

Tom Holland: Nikipata mtoto naacha kuigiza

 Tom Holland: Nikipata mtoto naacha kuigiza


Mwigizaji maarufu wa Hollywood, Tom Holland, amezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kusema kuwa siku atakapokuwa baba, ataacha kuigiza au atapunguza kabisa kufanya shughuli hizo ili aweze kuzingatia familia yake kwa karibu.

Holland amefunguka hayo wakati alipokua kwenye mahojiano na jarida la Men’s Health, akieka wazi kuwa baba ndio kipaumbele chake cha maisha, zaidi ya umaarufu au kazi ya uigizaji.

Mwigizaji huyo ambaye ametambulika Zaidi kupitia filamu ya Spider-Man alisema “Siku nitakapokuwa na watoto, hutawahi kuniona kwenye filamu tena. Golf na maisha ya nyumbani ndiyo nitakayojishughulisha navyo. Nitapumzika kabisa sitoonekana katika filamu yoyote.

Uamuzi wake umeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo kwa kuwa mtu anayejua kupanga maisha yake pamoja na kuweka vipaumbele.

Holland kwa sasa anaendelea na kazi zake kadhaa za filamu huku kukiwa bado kunatetesi kuwa yeye na mpenzi wake wa muda mrefu Zendaya kuwa wmefunga ndoa.

Tom Holland na Zendaya walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa wakishiriki kuigiza filamu ya Spider-Man: Homecoming mwaka 2016. Tangu hapo urafiki wao ulianza kuvutia mashabiki wengi, huku wengi wakihisi kuwa kuna zaidi ya urafiki kati yao.

Hatimaye mwaka 2021 walithibitisha rasmi uhusiano wao baada ya picha zao wakibusiana ndani ya gari kusambaa mitandaoni, na tangu wakati huo wameendelea kuwa katika mahusiano yanayovutia mashabiki wengi duniani.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.