Aendelea kushikilia rekodi ya kuwa na miguu mikubwa zaidi

Mwanaume mmoja kutoka mji wa Maracay nchini Venezuela, Jeison Orlando Rodríguez Hernández, aliweka historia mwaka 2018 baada ya kutambuliwa na Guinness World Records kwa kuwa na miguu mikubwa zaidi duniani. Ambapo hadi sasa anashikilia rekodi hiyo, mguu wake wa kulia una urefu wa sentimita 40.55 huku wa kushoto ukiwa sentimita 40.47.
Jeison anasema aligundua tofauti hiyo tangu alipokuwa na umri wa miaka tisa, wakati akilinganisha ukubwa wa miguu yake na marafiki zake. Mara nyingi walikuwa wakipima ukubwa wa miguu yao kwa utani, lakini kila wakati yeye ndiye aliyekuwa na miguu mikubwa zaidi kuliko wote.

Hata hivyo, ukubwa huo wa miguu haukuwa rahisi kwake katika maisha ya kila siku. Wakati mwingine alikuwa akichekwa na watu waliomzunguka, huku changamoto kubwa ikiwa ni kupata viatu vinavyomtosha katika mji wake wa Maracay. Kutokana na hali hiyo, mara kadhaa alilazimika kuvaa viatu vya wazi vilivyotengenezwa kwa kutumia matairi.
Baadaye alipewa heshima ya kukabidhiwa rasmi rekodi yake katika duka la viatu la Wessels Shoe Store, lililopo nchini Germany. Katika duka hilo, mmiliki wake Georg Wessel alimtengezea viatu maalum kwa sababu ukubwa wa miguu yake ni mkubwa sana kiasi kwamba viatu vya kawaida haviwezi kumtosha.
Inafahamika pia kuwa Wessel amewahi kutengeneza viatu kwa Sultan Kösen, ambaye anashikilia rekodi ya mtu mrefu zaidi duniani aliye hai, ingawa ukubwa wa miguu yake ni mdogo kidogo ukilinganishwa na wa Jeison.

Kwa mujibu wa taarifa za Guinness, Jeison aliwasiliana nao kupitia ukurasa wao wa Facebook na baadaye rekodi yake ya kipekee ikathibitishwa rasmi, jambo lililomfanya kuwa mmoja wa watu wanaovutia zaidi katika orodha ya rekodi za dunia.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.