Tetesi za Soka Ulaya : Chelsea kuharakisha usajili wa Messi
Chanzo cha picha,
Chelsea inaweza kuharakisha mipango ya kumsajili winga wa Ufaransa Rayane Messi, 18, kutoka Strasbourg huku Bayern Munich, Barcelona na Paris St-Germain pia zikimtaka. (Teamtalk)
Maajenti kutoka Manchester City, Liverpool, Arsenal, RB Leipzig, Borussia Dortmund na Barcelona wanamfuatilia kwa karibu beki raia wa Uingereza na timu ya Newcastle, Lewis Hall mwenye umri wa miaka 21. (Caughtoffside)
Manchester City pia inaweza kumsajili beki wa Uhispania, Pedro Porro, 26, kwa bei ya chini sana kuliko thamani yake ya pauni milioni 80 kutokana na hali ya kifedha ya Tottenham ikiwa watashushwa daraja. (Football Insider)

Sunderland wako tayari kulipa euro milioni 15 (£12.9m) ili kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania, Thiago Pitarch, 18, kutoka Real Madrid. (Fichajes)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.