Kweli Diamond ameiga video ya Bruno Mars

Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na mijadala ikidai kuwa video ya wimbo wa ‘Happy’ kutoka kwa mwanamuziki Diamond Platnumz inalingana kabisa na ile ya ‘24K Magic’ kutoka kwa Bruno Mars.
Baadhi ya watu walioangalia video hizo mbili wanaeleza kuwa kuna mfanano katika video ya Bruno na Simba ikiwemo miondoko ya dansi, aina ya mavazi, pamoja na muonekano wa kifahari unaotawala ndani ya video zote mbili.
“24K Magic” uliyoachiwa miaka 9 iliyopita huku ukitazamwa Zaidi ya mara 1.7 bilioni unajulikana kwa kuonyesha maisha ya kifahari, starehe na burudani ya hali ya juu, kitu ambacho pia kinaonekana katika video ya wimbo wa“Happy”.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mashabiki na wadau wa burudani wamekuwa wakimnanga Simba kwa kuiga na ku-copy matukio mbalimbali kutoka katika video ya Bruno huku wengine wakimsema kuwa ameishiwa ubunifu.
Hata hivyo baadhi yao wamekuwa wakimtetea msanii huyo wakieleza kuwa suala hilo ni la kawaida kwani mastaa wengi hutazama kazi za wengine waliotangulia au wanaofanya vizuri ili kujifunza mbinu mpya za ubunifu.
Aidha hii si mara ya kwanza kwa Diamond Platnumz kudaiwa kuiba mitindo ya wasanii wengine. Awali amewahi kudaiwa kuwaiga mastaa kama Chris Brown kwenye upande wa dansi, Asake katika ubunifu wa video, pamoja na marehemu Michael Jackson kutokana na uchezaji wake jukwaani.
Video ya wimbo huo tayari imetazamwa Zaidi ya mara milioni 2,ikiwa ni siku tatu tu tangu kuachiwa kwake, huku ikishika nafasi ya kwanza katika mtandao wa YouTube.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.