Bifu la Nicki Minaj, Cardi B linamchango gani kwenye hip hop

Hiphop ni moja ya muziki uliyoshika kasi tangu miaka ya 1980 ukiibua wasanii wengi hasa wa kiume. Kuanzia kina Will Smith, LL Cool J, MC Hammer, 2Pac Shakur, Notorious BIG, DR Dre, Snoop Doggy, Nas, Jay z, Buster Rhymes na makundi mengi yakiwamo Naughty By Nature, Refuge, Lost Boys, Public Enemy na mengine mengi.
Baadhi ya wasanii wakaingia katika chat kutokana na muziki huo na wengine wakishindanishwa kutokana na ubora wao.
Miaka hiyo ya 80 pia kuliibuka wasanii wa kike waliotikisa miondoko hiyo wakiwamo Roxanne Shante na Sparky D, MC Lyte, Queen Latifah, Salt-N-Pepa, Missy Elliott, Lil' Kim, Foxy Brown, Da Brat, Lauryn Hil, Eve, Lisa 'Left Eye' Lopes, Rah Digga na wengine wengi.
Kuwepo kwa ushindani wa kuchana kukaibua bifu kwa baadhi ya wasanii na wengine kusaabisha madhara ikiwamo vifo kama ilivyokuwa kwa wakali 2Pac na BIG na wengine wakiishia kurushiana vijembe katika mashairi yao.
Wapo wengi waliofanya hivyo wakiwamo Nas na Jay Z, 50 Cent na Jah Role na wengineo.
Uwepo wa bifu hizo ukaonekana kama sehemu ya kuidumisha Hiphop na hadi sasa imekuwa ikiendelea kwa wasanii wa kizazi hiki wakiwamo Drake na kendrick Lamar na mabifu mengine.
Kwa upande wa wanawake wa kizazi cha sasa, kumekuwa na mvutano wa nani mkali baina ya marapa wawili, Nicki Minaj na Cardi B na mashabiki wao wamwekuwa wakiwasapoti kuongeza ubora wao na ndo hapo kila upande unaona wao ndio zaidi.
Bifu zimekuwa zikiwabeba wasanii hasa kibiashara na wawili hawa wamepata mafanikio na ushawishi kwa jamii huku wakizidiana baadhi ya mambo.
Makala haya yanachambua uhasama, rekodi, mafanikio na ushawihi wa kila mmoja kwa kuzingatia namna Nicki aliyeweka historia huku Cardi B aliyemkuta mwenzake kwenye game akiendeleza kwa kuwa na ushawishi mkubwa mitandaoni.
Uhasama wa muda mrefu kati ya Nicki Minaj na Cardi B uliibuka tena mnamo Septemba 2025 baada ya kutoka kwa albamu ya Cardi B ya Am I the Drama? Uhasama huo ulihusisha majibizano kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na shutuma kuhusu mauzo ya albamu, maisha ya kibinafsi, na matusi yaliyowahusisha watoto wao na kuashiria kuongezeka kwa ugomvi wao wa miaka mingi.
REKODI ZA NICKI
Nicki Minaj amejijengea historia kwenye muziki wa Hiphop sio kwa rekodi zake pekee bali pia namna alivyobadilisha kabisa tasnia ya hip hop kwa wanawake.
Kabla ya Nicki kulikuwa na wasanii wachache wa kike lakini hawakuonekana kufanya vizuri zaidi alipokuja mwishoni mwa mwaka 2000 na alionekana kurudisha nguvu ya wanawake kwenye hiphop.

Wasanii wengi wa kizazi kipya kama Cardi B, Megan Thee Stallion na Doja Cat wamefaidika na njia aliyofungua mwanadada huyo aliyetamba na kibao cha 'Super Bass'.
Mkali huyo ana rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike nyimbo zake nyingi kuingia kwenye chati ya Billboard Hot 100 zikashindana na wasanii kama Jay Z, Lil Wayne, Drake na wengineo.
Mwanamke wa kwanza kufikisha nyimbo 100+ kwenye Billboard Hot 100. Hii ni rekodi kubwa sana kwenye historia ya muziki wa hip hop na bado rekodi hiyo haijavunjwa na msanii yeyote wa kike.
Mwaka 2010 alitoa albamu yake ya kwanza Pink Friday iliyofanya vizuri na kushika namba moja kwenye Billboard 200. Ni msanii wa kwanza wa kike wa rap kufikisha watazamaji zaidi ya bilioni 1 kwenye mtandano wa Spotify.
Kwa upande wa tuzo amenyakua tuzo 45 zikiwemo tisa za American Music, BET akichukua 11, MTV Video Music amebeba nane, MTV Europe Music (12) na Billboard Music tano.
Licha ya kuufanya muziki huo kwa zaidi ya miaka 20 lakini hajachukua tuzo kubwa za muziki duniani Grammy akiwania mara 12.
CARDI B NAYE
Mwanadada huyo aliingia kwenye tasnia hiyo kwa kasi mwanzoni mwa mwaka 2015 na wala hakuchukua muda akawa maarufu kutokana na aina yake ya kurap.
Kazi yake ya kwanza kuifanya kama msanii wa rap alishirikishwa kwenye ngoma ya Shaggy iitwayo 'Boom Boom'.
Baada ya remix hiyo akaendelea kutoa ngoma ambazo zilienbdelea kufanya vizuri kama 'Money' iliyotoka miaka saba iliyopita ikiwa na zaidi ya watazamaji Milioni 100 'I like it' ikipiga zaidi ya watazamji Bilioni na kuandika rekodi ya ngoma yake kutazamwa zaidi.
Pamoja na kuwa na baadhi ya nyimbo zilizofanya vizuri na kushika chati za juu za muziki lakini Cardi B ana rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike kushinda tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha Albamu bora ya rap akichukua kupitia albamu ya 'Invasion of Privacy' mwaka 2019.
Mwaka huo akashinda tuzo za Billboard Music kama msanii bora wa kike wa rap, miaka miwili baadae akanyakua tuzo za American Music.
Kwa jumla Cardi B ana tuzo 23 kwenye kabati lake, moja ya Grammy, nane za BET, sita za Billboard na nane za American Music.
ALICHOMZIDI NICKI
Kilichofanya Cardi afanikiwe kwa haraka ni kutokana na namna ya kutumia mitandano ya kijamii kama Instagram na TikTok kufanya promo ya nyimbo zake jambo ambalo limeiwezesha ngoma hizo kuenea kwa kasi.
Pia namna yake ya kusambaza mziki amekuwa akitumia kiki na muda mwingine kufanya chalenji za kuingia hadi mtaani kukutana na mashabiki zake na kuuza kazi zake.
Kuzingatia rekodi, historia na ushawishi, Nicki ni mhimili wa Hiphop ya wanawake ambaye amekuwa na muendelezo wa kazi na kudumu kwa muda mrefu bila kushuka.
Cardi ni msanii mwenye ushawishi mkubwa kwa kipindi hiki na pamoja wanathibitisha wanawake wanaweza kushindana na wanaume kwenye muziki ulioonekana ni wababe na watu wagumu ndio pekee wanaoweza kuufanya.
BIFU LIKО НАРА
Mbali na kushindanishwa na mashabiki, wenyewe wamekuwa wakikoleza bifu lao kwa kutambiana mitandaoni na vyombo vya habari juu ya nani mkali.
Tofauti namiaka ya nyuma wasanii wa kike waliimarika kwa vijembe na matusi katika kuchana na hakukuwa na mitandao ya kuwafanya mashabiki waingilie kwa kiasi kikubwa zaidi ya kukutana stejini, kwa Nicki na Cardi B pia ni sehemu ya kujiongezea mafanikio ya kiuchumi na kukusanya kijiji na wamekuwa wakiendelea kurushiana vijembe kila mara.
Kwenye moja ya posti aliyoichapisha Nicki aliandika "sasa tuanze hapa hivi... Mimi ndiye ndiye ninaongoza kwa kila kitu," akisisitiza kuwa ndiye msanii anayekuwa juu na kuongoza.
Cardi alijibu "Kwa muda sasa amekuwa akinipiga mishale mingi kila mmoja afanye yake huu ni wakati wangu," anasema.
Pia wamekuwa wakitumia hadi ngoma zao kurushiana vijembe jambo linaloelezwa kwa kiasi kikubwa limeongeza ufuatiliaji kwa wasanii hao.
Moja ya majibishano yao kwenye ngoma zao ni; "ABCDEF G, mumeo lazima achukuliwe, kaka yako anagusa watoto wa miaka 12," alisema Cardi B akitumia mstari wa wimbo wa Nicki kumkosoa na familia yake.
Nicki alijibu "ABCDEFG... umeshuka kwenye chati huko na tumbo kubwa... Hata hivyo, huwezi kuinuka na kunipita kwa mauzo."

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.