-->

Breaking News

Shreya Ghoshal naye afikiria kuacha muziki

 Shreya Ghoshal naye afikiria kuacha muziki

Mwimbaji maarufu wa muziki wa filamu za Kihindi, Shreya Ghoshal, amefunguka kwa mara nyingine kuhusu changamoto za kazi yake, akieleza kuwa nayeye anafikiria kuacha kuimba kwa muda.

Akizungumza katika mahojiano na ABP News, Shreya ambaye ametambulika kupitia wimbo wa Devdas, alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya afikirie kuacha kuimba ni kutokana na presha na mzigo wa kazi ya muziki.

“Mimi pia nafikiria kupumzika kuimba. Nadhani Arijit Singh alifanya uamuzi huo kwa ujasiri mkubwa... Yeye ni mwanamuziki anayeimba kwa moyo. Hafikirii kwa nini anafanya muziki au atapata nini kutokana na hilo. Yeye hufanya tu kile kinachomfurahisha,”amesema

Aidha kauli hiyo ya kutaka kuacha kuimba, imekuja wakati ambao kumejaa mjadala kutoka kwa mashabiki wakiendelea kudodosa sababu ya Arijit Singh kuacha kuimba ambapo Shreya alieleza kuwa Singh alifanya uamuizi huo kwa ujasiri na kwa moyo wa kisanii.



Ikumbukwe Arijit Singh alitangaza kuacha uimbaji wa playback Januari 27,2026 . Katika tangazo hilo, alisema hatachukua tena kazi mpya kuanzia muda huo na kuwa ataendelea kushiriki katika baadhi ya miradi ambayo bado hajaikamilisha.

Aidha, Shreya aligusia pia suala la uigaji wa sauti (lip-sync) katika matukio ya live, akieleza kuwa hali hiyo haimfurahishi. Huku akisema wazi kuwa siku atakayolazimishwa kufanya lip-sync basi yupo radhi kutotumbuiza.

Kauli zake zimeibua mjadala mpya katika tasnia ya muziki, huku mashabiki wakibaki na sintofahamu wakishindwa kuelewa ni sababu zipi zinazowafanya wasanii hao kuanza kujiondoa mmoja baada ya mwingine katika tasnia hiyo.

Shreya Ghoshal alianza safari yake ya muziki akiwa tangu mtoto ambapo alipata umaarufu mwaka 2002 baada ya kushinda katika mashindano ya kuimba ya Sa Re Ga Ma Pa (Zee TV), mashindano ambayo yalimfungulia milango rasmi ya kuingia katika tasnia ya muziki wa filamu (playback singing).

Baada ya ushindi huo, alipata nafasi ya kufanya kazi yake ya kwanza katika filamu ya Devdas iliyotoka 2002, ambapo aliimba nyimbo zilizomfanya atambulike haraka kila kona ya India na duniani kwa ujumla.

Shreya ambaye amekuwa akifahamika kwa sauti yake ya kipekee kupitia nyimbo mbalimbali zikiwemo “Bairi Piya” –Devdas, “Dola Re Dola” – Devdas, “Jaadu Hai Nasha Hai” – Jism, “Teri Ore” – Singh Is Kinng, “Manwa Laage” – Happy New Year, “Sun Raha Hai (Female Version)” – Aashiqui 2 “Nagada Sang Dhol” – Goliyon Ki Raasleela Ram-Leela, “Deewani Mastani” – Bajirao Mastani, “Ghoomar” – Padmaavat, “Chikni Chameli” – Agneepath, “Agar Tum Mil Jao” – Zeher, “Radha” – Student of the Year na nyinginezo.

Kutokana na kipaji chake amefanikiwa kutunukiwa na kunyakuwa tuzo mbalimbali zikiwemo za National Film Awards, Filmfare Awards ambazo ni miongoni mwa tuzo kubwa za Bollywood, Filmfare Awards South, IIFA Awards (International Indian Film Academy Awards, Zee Cine Awards, Mirchi Music Awards, Asianet Film Awards pamoja na Global Indian Music Academy (GiMA) Awards.


Shreya Ghoshal anakadiriwa kuwa na utajiri wa takribani dola za Marekani milioni 25–30, ambao unatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo uimbaji wa playback katika filamu za Bollywood na lugha nyingine, matamasha ya moja kwa moja ndani na nje ya India, matangazo ya bidhaa (brand endorsements), pamoja na mapato ya mitandao ya kidijitali kama YouTube na streaming, ambapo kwa miaka mingi amekuwa miongoni mwa waimbaji wanaolipwa vizuri zaidi kutokana na umaarufu wake na ubora wa sauti yake.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.