Mfahamu Uche Montana, mwigizaji anayetikisa Nollywood kwa sasa

Katika ulimwengu wa burudani, si kila anayeanza safari ya sanaa hufanikiwa kufika kileleni. Wengi huanza kwa ndoto kubwa lakini hukwama njiani kutokana na changamoto mbalimbali.
Hata hivyo, kwa mwigizaji kutoka Nigeria, Uche Montana, imekuwa tofauti kwani kwa upande wake uthubutu, nidhamu na juhudi zimemfanya kuingia kwenye orodha ya waigizaji wanaokubalika Zaidi katika tasnia ya filamu Barani Afrika.
Uche Montana, ambaye jina lake halisi ni Uche Nwaefuna, alizaliwa Aprili 8, 1994 nchini Nigeria. Amesoma katika Chuo Kikuu cha Lagos akichukua kozi ya Business Administration. Ingawa alichukua kozi hiyo ya biashara lakini mapenzi yake kwenye sanaa ndiyo yaliyomvuta zaidi na hatimaye kuamua kuingia kwenye tasnia ya Nollywood.

Baada ya kuwa na ndoto ya kuingia katika tasnia ya filamu tangu alipokuwa mdogo, ndoto hiyo ilianza kutimia taratibu ambapo safari yake ya uigizaji ilianza rasmi mwaka 2016 alipopata nafasi katika tamthilia maarufu iitwayo Hush.
Hii ilikuwa hatua muhimu iliyofungua milango ya mafanikio yake, kwani kupitia kazi hiyo aliweza kuonesha uwezo wake mkubwa wa kuigiza na kuvutia macho ya wadau wa tasnia ya Nollywood.
Baada ya hapo, alianza kuonekana kwenye filamu na tamthilia mbalimbali, akijizolea umaarufu hatua kwa hatua. Umahiri wake katika kuvaa uhusika kwenye drama za maisha halisi ulimfanya kupendwa Zaidi na mashabiki hasa wa kizazi cha sasa ‘Gen Z’ kinachopendelea maudhui ya mapenzi (mahusiano).
Aidha ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya namna ya usambazaji wa filamu ulivyo umefungulia milango mingine muhimu. Ambapo mwaka 2024 alifungua chanel yake ya Youtube ijulikanayo kama ‘Uche Montana TV’ kupitia jukwaa hilo alifanikiwa kuwafikia mashabiki wake katika pande mbalimbali za dunia, ambapo mpaka kufikia sasa chaneli hiyo inazaidi ya wafuatiliaji 1.35 milioni.
Hata hivyo moja ya filamu ambayo inafuatiliwa Zaidi kwasasa na ambayo imepata watazamaji wengi ni ‘Monica, A True Life Story’ iliyotazamwa mara 12 milioni ikiwa ni wiki mbili tuu zimepita tangu kuachiwa kwake.
Mwanzoni, safari hiyo haikuwa rahisi. Ushindani ulikuwa mkubwa, lakini alizingatia mambo kadhaa muhimu ikiwemo ubora wa hadithi, mwendelezo wa utoaji wa maudhui yanayoendana na maisha halisi, pamoja na kushirikiana na waigizaji wengine maarufu. Hatua hizo zilifanya channel yake kuanza kuvutia watazamaji wengi na hatimaye kujikusanyia mamilioni ya mashabiki duniani kote.
Katika upande wa uandishi wa stori, Uche Montana hafanyi kazi peke yake. Kama ilivyo kwa wasanii wengi wa Nollywood, hushirikiana na waandishi mbalimbali wa script kulingana na mradi husika. Jambo ambalo humwezesha kupata mitazamo tofauti ya ubunifu na kuleta utofauti katika kazi zake. Aidha, ingawa si mwandishi mkuu wa kazi zake zote, hushiriki katika kuchagua na kuboresha stori ili ziendane na hadhira yake.
Kuhusu Mahusiano
Licha ya mafanikio yake, Uche Montana ameendelea kuwa msanii anayelinda sana maisha yake binafsi. Tofauti na baadhi ya mastaa wanaoweka wazi mahusiano yao, yeye amechagua kuyaweka faragha, hali inayoongeza mvuto na kuibua maswali miongoni mwa mashabiki wake.
Aidha zipo tetesi kuwa maisha yake yanaendeshwa na sponser, lakini wakati alipokuwa akizungumza na mashabiki zake alikanusha suala hilo alieleza kuwa maisha mazuri na kuishi kwakwe kifahari kunatokana na kufanya kazi kwa bidii.

“Kumekuwa na dhana nyingi potofu watu wakiuliza napataje pesa Wapenzi wangu, tupo katika kipindi ambacho unaweza kutengeneza pesa kupitia tasnia hii, na ninajivunia kusema mimi ni mmoja wa watu wanaopata kipato kupitia tasnia hii, na napenda kujifurahisha.
“Nafanya kazi kwa bidii, na pia najifurahisha. Kwa kweli, nafanya kazi zaidi kuliko ninavyojifurahisha. Lakini kuna uwiano, kwa sababu mwisho wa siku mimi ni msichana mdogo, nahitaji pia kuunda kumbukumbu maishani. Ni muhimu sana kuunda kumbukumbu ambazo siku moja nitawaambia watoto wangu, nilifanya hiki na kile wakati Fulani,”alisema Uche
Mpaka kufikia sasa ameshaachia filamu mbalimbali katika chanel yake hiyo ikiwemo A Place With You (2026), Nine Months Till Forever, Hustle Code, Chaos to Calm, A Lady and Her Gentleman, Love Pursuit, Six Months of Grace, Baby Blues na nyinginezo. Huku mashabiki wakisubiri kwa hamu mwendelezo wa filamu ya Monica inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.