-->

Breaking News

Kisa ubaguzi, anunua kila kilemba na Rolls-Royce yake

 Kisa ubaguzi, anunua kila kilemba na Rolls-Royce yake

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Mwaka 2017 mfanyabiashara tajiri mwenye asili ya India anayeishi Uingereza, Reuben Singh, alizua gumzo mitandaoni baada ya kuonesha jeuri ya pesa kutokana na kejeli za watu.

Inaelezwa kuwa baadhi ya watu nchini humo walikuwa wakimtolea maneno ya ya kibaguzi kufuati mavazi aliyokuwa akiyavaa. Ndipo aliamua kuwajibu kwa njia ya kipekee iliyopelekea kuzuka gumzo zaidi.



Katika mitandao ya kijamii watu walimkejeli kwa uvaaji wake wa kilemba wakiandika “watu wanaovaa turban hawawezi kuwa na mafanikio makubwa.” Huku wengine wakimdhihaki kwa kuandika “Wanaovaa vilemba ni wanawake tuu”. Kauli hiyo haikumdhoofisha, bali ilimpa motisha ya kuonyesha mafanikio yake kwa vitendo.



Singh aliamua kuanzisha challenge yake iitwayo ‘Rolls-Royce Turban Challenge’ ambapo kila siku ndani ya siku saba alivalia kilemba cha rangi inayofanana na gari yake ya kifahari aina ya Rolls-Royce.

Ndani ya siku hizo Saba, Singh alipiga picha akiwa amesimama mbele ya magari yake ya kifahari 'Rolls-Royce' yenye rangi mbalimbali kama nyekundu, bluu, njano, kijani na nyinginezo.

Picha hizo zilianza kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii. Huku watu wengi wakivutiwa na ujumbe uliokuwa nyuma ya hatua hiyo: kujivunia utamaduni wako na kujibu ubaguzi kwa mafanikio badala ya hasira.



Singh, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uwekezaji ya Isher Capital, tayari alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa kabla ya tukio hilo. Hata hivyo, “Rolls-Royce Turban Challenge” ilimfanya ajulikane zaidi duniani kote huku ikiongeza wawekezaji zaidi katika kampuni yake.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.