Dharau, majivuno zilivyozima jina la msanii Ranu Mondal

Kuna methali inasema 'Mwanga wa mshumaa hudumu kwa muda mfupi' nyingine inaeleza 'Kila penye mwanzo kuna mwisho', zikiwa na maana kila jambo linaweza kuisha kwenye hii dunia, ikiwamo umaarufu.
Methali hizi zinalandana na kisa cha mwanamama, Ranu Mondal mwanamuziki kutoka India ambaye alipata umaarufu na baadae ukapotea.
Simulizi yake inayogusa hisia kutoka kuwa mtu wa kawaida hadi kuwa supastaa wa ghafla, kisha baadae kurejea kwenye maisha ya kawaida yenye changamoto kubwa. Ni mfano halisi wa msemo unaosema, umaarufu wa mtandaoni ni wa muda mfupi.
Mwaka 2019 Mondal alipata umaarufu mkubwa baada ya video yake akiimba wimbo wa "Ek Pyaar Ka Nagma Hai" katika kituo cha treni kusambaa mitandaoni.

Ndani ya muda mfupi, alialikwa kushiriki kwenye vipindi vya televisheni na hata kupewa nafasi ya kuimba na nyota wa Bollywood, Himesh Reshammiya kwenye ngoma ya 'Teri Meri Kahani'.
Ngoma na Reshammiya ilimfanya kuwa maarufu na kuanza kupata madili ya kuimba sehemu mbalimbali, pia sauti yake ilisikika kwenye filamu za India ikiwemo 'Happy Hardy and Heer'.
Alifanya pia kolabo na wasanii wengine akiwemo nyota wa Bangladesh, Hero Alom na kuwa gumzo kubwa mitandaoni.
UMAARUFU
Kama ilivyo kwa wengine mtu anapopata mafanikio baadhi yao hupata kiburi Mondal akaanza kuvimba kuanzia kwa mashabiki hadi wale waliompa nafasi ya kuonekana.
Mafanikio hayo yalikuja kwa kasi ambayo pengine hayakumpa nafasi ya kujiandaa kwani alitoka katika maisha ya kawaida hadi kuwa mtu anayefuatiliwa na vyombo vya habari, mashabiki na mitandao ya kijamii kwake ilikuwa jambo geni kabisa.
Alianza kutoa ngoma mbalimbali zilizoendelea kufanya vizuri kama 'Aadat', 'Small' na kutokana na sauti yake aliendelea kupata mashabiki wengi zaidi ndani na nje ya India.
Mashabiki hao hao waliokuwa wanamfuatilia akaanza kuonyesha tabia zisizo za kawaida muda mwingine hata kuomba picha ilihitaji ujasiri wa hali ya juu kutokana na namna anavyoonyesha kiburi.
Kuna matukio ya majivuno na dharau aliyaonyesha hadi kwa Reshammiya supastaa aliyefungua milango ya kipaji chake hadi watu kumfahamu.
Mondal kwenye moja ya mahojiano alisema "Kunifananisha na Reshammiya ni kitu cha ajabu, nishakuwa mtu maarufu unanilinganishaje naye," alinukuliwa.
Video hiyo ilisambaa mitandaoni kila mmoja akizungumza lake na wengine wakisema nidhamu ni jambo muhimu kwenye maisha hata kama unamzidi mtu fulani kwa mali.
Wengine walimtetea huenda hana wasimamizi wazuri wa muziki wake, wakiamini anatumia maneno hayo ili azidi kuwa maarufu na kufuatiliwa na watu.
MAISHA YA SASA
Miaka mitano ya umaarufu na raha iligeuka kuwa michungu kwa msanii huyo mwenye sauti ya kipekee, baadhi ya ripoti zilieleza amerudi kwenye maisha yake ya kawaida.
Ripoti za tabia ya ukali kwa mashabiki na waandishi wa habari inaelezwa zilichangia kupungua kwa umaarufu wake. Taswira ya msanii ni mtaji mkubwa mashabiki wanapohisi kukataliwa au kudharauliwa, uhusiano huvunjika haraka.
Mwishoni mwaka 2025, Ranu inaelezwa anaishi tena West Bengal katika mazingira magumu, Video zilizorekodiwa na watu waliomtembelea zinaonyesha, nyumba yake ikiwa katika hali duni, hakuna mpangilio wa vyombo na kukosa mahitaji ya msingi kama vyombo vya kuhifadhia chakula na kutegemea wageni wanaomtembelea wampe pesa kwa ajili ya matumizi na kulipa madeni.
AFYA YA AKILI
Majirani wa karibu wa msanii huyo wanaeleza ni kama ana changamoto ya afya ya akili kwani kuna muda anakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na wakati mwingine anapoteza fahamu.
Wanadai amekuwa akipitia msongo wa mawazo (stress) na kuishi peke yake kumechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na tatizo hilo kwani hana mtoto na tangu mumewe afariki dunia hakuna mtu wa karibu anayeishi naye.
WENGINE
India siyo mara ya kwanza kutokea hilo kwa wasanii, wapo waliopitia hali ya kushuka kifedha na umaarufu lakini hali ya Mondal inaelezwa imezidi.
Wasanii wengine wa Bollywood waliopata umaarufu na kurudi kwenye umaskini miongoni mwa ni Bhuban Badyakar alijulikana kupitia wimbo wa 'Kacha Badam' lakini alikumbana na changamoto ghafla.
Mubarak Begum, licha ya kuwa na historia kubwa ya muziki, aliishi maisha ya taabu katika uzee wake.
Kwa upande mwingine, wapo walioweza kuvuka changamoto hizo na kufanikiwa kwa muda mrefu, kama A. R. Rahman, ambaye licha ya kukulia katika umaskini, alifanikiwa kutokana na nidhamu, mipango na msaada wa watu wa karibu.
MAONI YA MASHABIKI
"Ninatoka Sri Lanka inasikitisha sana kuona hali ya sasa ya Ranu. Tunajua alifanya makosa kadhaa baada ya kupata umaarufu, lakini je, tunapaswa kusahau historia yake ngumu? Umaskini, njaa, na miaka ya upweke, Labda ilikuwa vigumu kwake kushughulikia umaarufu huu wa ghafla kwa sababu hajawahi kupata heshima au upendo maishani mwake," anaandika Manjula Priyantha.

"Binadamu wameumbwa kwa makosa, na Ranu pia ni binadamu. Je, hapaswi kupewa nafasi nyingine, kutokana na sauti yake tamu na magumu yake? Watu wa India wamekuwa na moyo mkuu kila wakati. Tafadhali usimwache msanii katika giza na umaskini kama huo. Mpe nafasi ya mwisho ya kuboresha na kuonyesha kipaji chake," anasema Shiva Awadh.
"Wako wapi watu wa India ambao hawachoki kujisifu kuhusu uimbaji wao na sauti zao tamu? Hata baada ya kuwaona katika hali hii, mioyo yao haikuyeyuka kwa shida yao. Kwa nini? Je, ni kwa sababu wao ni wafanyakazi maskini?," anaandika Krishna Priya
"Hadithi ya Ranu Mandal inatufundisha kwamba kipaji hakitegemei hali. Ikiwa kipaji ni cha kweli na fursa inapatikana kwa wakati unaofaa, hata hatima inaweza kubadilika. Maisha yake ni mfano wa mapambano, uvumilivu na matumaini," anaeleza Ravinder Kaur.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.