-->

Breaking News

Usher na Justin Bieber wataka kuzichapa

 Usher na Justin Bieber wataka kuzichapa

Wanamuziki Usher na Justin Bieber waliripotiwa kutaka kuzichapa katika sherehe ya baada ya tuzo za Oscar (after-party) iliyoandaliwa na mastaa Beyoncé na Jay-Z.

Kwa mujibu TMZ wawili hao walihusishwa na mabishano yenye kelele ambayo yaliyosababisha sintofahamu miongoni mwa waliohudhuria, huku baadhi ya vyanzo vikidai kuwa walifikia hatua yakutaka kuingiana maungoni (kupigana).

Chanzo kimoja kilicho karibu na Bieber kimeiambia TMZ kuwa Usher ndio alimfuata msanii huyo akiwa na hasira, hali iliyopelekea majibizano makali, lakini hakukuwa na mgusano wa kimwili licha ya hali kuwa ya mvutano mkubwa. Hata hivyo, upande wa Usher haujatoa tamko rasmi kuhusiana na tukio hilo.

Aidha, taarifa zinaeleza kuwa Justin Bieber amekuwa akijaribu kujitenga na baadhi ya watu wa zamani katika maisha yake, huku chanzo kingine kikidai kuwa mara kadhaa amekuwa akionesha ukorofi kwa Usher, ambaye aliwahi kuwa mlezi wake kisanaa mwanzoni mwa safari yake ya muziki.

Pamoja na hayo, bado haijabainika chanzo halisi cha mzozo huo, ingawa inaelezwa kuwa haukudumu kwa muda mrefu. Tukio hilo linaelezwa kushuhudiwa na idadi kubwa ya watu maarufu, kutokana na sherehe hiyo kuhudhuriwa na mastaa wengi wakubwa duniani.

Miongoni mwa waliohudhulia ni pamoja na Taylor Swift, Travis Kelce, Michael B. Jordan, Ryan Coogler, Teyana Taylor, Timothée Chalamet, Kylie Jenner, Austin Butler, Jacob Elordi, Emma Stone, Emma Watson, Kendall Jenner, Megan Fox, Kris Jenner, Sofía Vergara, Vin Diesel, Jon Batiste, Jack O'Connell, Chloe Bailey, Vanessa Bryant na Natalia Bryant, pamoja na mke wa Bieber, Hailey Bieber.



Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho wawili hao kuonekana pamoja wakiwa washkaji ilikuwa mwaka 2022 katika Coeur d’Alene, jimbo la Idaho, nchini Marekani.

Usher ni mmoja wa wasanii ambao walisaidia kukitambulisha kipaji cha Bieber ambapo alimsaidia kusainiwa na kampuni ya muziki ya Island Records baada ya kumuona kupitia video zake za YouTube. Wakati huo, Bieber alikuwa bado kijana mdogo akiwa na umri wa miaka 14.

Mbali na hilo Usher pia alimlea kisanaa (mentor) alimfundisha mambo ya jukwaani, nidhamu ya kazi, na jinsi ya kujiendesha kama msanii mkubwa. Pia alimsaidia kupata nafasi za kurekodi nyimbo na kushirikiana na watu wakubwa kwenye muziki.

Zaidi ya hayo, Usher alimpatia Bieber mwonekano (exposure) kwa kumtambulisha kwa hadhira kubwa na kumshirikisha katika miradi mbalimbali, huku wakishirikiana kutoa wimbo uitwao Somebody to Love (Remix) (2010) wimbo ambao ulifanya vizuri katika chati za muziki.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.