BASATA yamuita Bi. Halima kwa kukiuka maadili

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemuita msanii wa nyimbo za mduara, Bi. Halima Haji pamoja na meneja wake Rahma R. Pascal kufuatia kusambaa kwa kipande cha video ya muziki kinachodaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya BASATA, kikao hicho kilifanyika Machi 18, 2026, ambapo wahusika walifikishwa mbele ya Baraza na kukiri kosa hilo. Baada ya hatua hiyo, taratibu zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya sanaa nchini.
“Kufuatia kusambaa kwa "clip" ya video ya muziki isiyozingatia maadili ya Mtanzania, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limefanya mazungumzo na Bi. Halima Haji na Meneja wake Rahma R. Pascal tarehe 18 Machi, 2026 na wamekiri kufanya kosa hilo, hivyo hatua nyingine za kisheria zinaendelea kufuatwa,” imeeleza taarifa hiyo

Basata imeeleza kuwa itaendelea kufuatilia na kusimamia kwa karibu maudhui ya kazi za wasanii ili kuhakikisha yanazingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.
Aidha, Baraza hilo limetoa onyo kali kwa wasanii wote, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayekiuka miongozo iliyowekwa.
Ikumbukwe msanii huyo tayari ameshafanya kolabo ya wimbo uitwao ‘Pembe’ akishirikiana na Chino Kidd, wimbo ambao umetazamwa Zaidi ya mara 776K katika mtandao wa YouTube.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.