Baada ya kuvamiwa, Rihanna aongeza ulinzi

Baada ya mwanadada Robyn Rihanna Fenty 'Rihanna' kuvamiwa nyumbani kwake na mwanamke anayetambulika kwa jina la Ivanna Ortiz, inaelezwa msanii huyo ameongeza ulinzi binafsi kila anapokwenda.
Rihanna alivamiwa kwenye nyumba anayoishi na mpenzi wake ASAP Rocky iliyopo Orlando Florida, Marekani Machi 08 mwaka huu.
Ortiz alifyatua risasi nyumbani kwa msanii huyo maarufu duniani ndipo akamfungulia shtaka la kutaka kumjeruhi na sasa anashiliwa na polisi.
Sasa tangu tukio hilo litokee Rihanna hakuonekana hadharani zaidi ya kutokea mahakamani kwenye kesi ya mashtaka aliyoifungua.
Wawili hao jana walionekana wakitoka katika jengo moja jijini New York City wakiwa wametulia lakini wakizungukwa na ulinzi mkali takribani askari sita waliokuwa kila upande.
Mashuhuda waliowaona ASAP na Rihanna wamesema waliondoka haraka kuelekea kwenye gari lao aina ya SUV hwakutumia zaidi ya dakika tano.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rihanna na ASAP kuonekana hadharani pamoja tangu tukio hilo la kushtua lilipo tokea ambapo Ortiz alifyatua risasi kadhaa kwenye nyumba yao wakiwa ndani pamoja na watoto wao.
Inaelezwa Rihanna na ASAP wanaishi kwenye nyumba yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya Dola 14 milioni pamoja na watoto wao watatu RZA mwenye miaka mitatu, Riot Rose mwenye miwili na Rocki Irish Mayers wa miezi 5.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Machi 10 mwaka huu kwenye mahakama ya Los Angeles nchini humo na Ortiz anahukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Mbali na kesi hiyo Ortiz anakabiliwa na makosa mengine ikiwemo mashtaka 10 ya shambulio kwa kutumia bunduki na mashtaka mengine matatu ya kufyatua risasi.
Polisi wamegundua kuna baadhi ya machapisho ya vitisho ambayo Ortiz alikuwa akiyaposti kwenye mitandao ya kijamii yakimlenga Rihanna.
Katika chapisho moja kwenye mtandao wa X, Ortiz alia ndika: Uko hapo? ... niambie moja kwa moja badala ya kuzunguka na kuzungumza nami wakati sipo.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.