-->

Breaking News

Chimbuko, wapenzi kuitana Baby

 Chimbuko, wapenzi kuitana Baby

Mara nyingi watu wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi majina ya utani huzaliwa. “Baby” ni mojawapo ya majina maarufu zaidi duniani, ikitumika kuashiria upendo, ukaribu na hisia. Twende pamoja


Neno “baby” lilianza karne ya 14 katika lugha ya Kiingereza likimaanisha mtoto mchanga. Utafiti wa kamusi ya Oxford English Dictionary unaonyesha asili yake ni sauti zinazotoka kwa watoto wachanga wanapojifunza kuongea, kama “ba-ba” au “be-be”. Kadri muda ulivyosonga, watu walianza kulitumia pia kama jina la upendo, likimaanisha mtu anayependwa na kutunzwa.

Hata hivyo karne ya 20, neno hili lilienea zaidi kupitia muziki, filamu na tamaduni za pop. Nyimbo za mapenzi zilitumia “baby” kuashiria mtu wa pekee na wa karibu. Hii ilisababisha neno hili kuwa sehemu ya kawaida ya mazungumzo kwenye wapenzi, si tu kwa Kiingereza, bali duniani kote.

Wataalamu wa mahusiano, akiwemo Carol J. Bruess, wanasema kuwa majina ya utani husaidia kuimarisha uhusiano wa kihisia. Kuonyesha upendo na ukaribu, linafanya mahusiano yaonekane ya pekee. Husaidia wapenzi kuelewana zaidi kihisia. Huwa anakuita baby?

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.