Utafiti: Miaka 27 ni muda mzuri wa ndoa, kupata mtoto

Kutokana na utafiti uliochapishwa katika jarida la kisayansi la Human Reproduction ulioongozwa na mwanasayansi David Dunson kutoka National Institute of Environmental Health Sciences. Ulionesha wanawake wenye umri wa miaka 19–26 walikuwa na takribani asilimia 50 ya nafasi ya kupata ujauzito katika mzunguko mmoja wa hedhi.
Kwa wanawake wenye umri wa miaka 27–34, nafasi hiyo ilishuka hadi karibu asilimia 40.
Kwa wanawake wenye miaka 35 na zaidi, nafasi ya kupata ujauzito hupungua hadi karibu asilimia 30 au chini kabisa
Matokeo haya yanaonyesha kuwa uwezo wa uzazi huanza kupungua polepole kuanzia miaka 27, na kushuka kwa kasi zaidi baada ya miaka 35.
Utafiti mwingine uliofanywa na watafiti W. Hamish B. Wallace na Thomas W. Kelsey umeonyesha wanawake huzaliwa na idadi maalum ya mayai ya uzazi ambayo hupungua kadri umri unavyoongezeka. Watafiti hao walikadiria kuwa kufikia umri wa miaka 30, wanawake wengi hubakiwa na sehemu ndogo tu ya akiba ya mayai waliyokuwa nayo tangu kuzaliwa.
Mbali na sababu za kibaiolojia, watafiti wa saikolojia ya mahusiano pia wanaona kuwa kuanzia miaka 27 ni kipindi ambacho watu wengi huwa wamepata utulivu zaidi wa maisha. Kwa wakati huo mara nyingi mtu huwa tayari amemaliza masomo, ameanza kujijenga kiuchumi na ana ufahamu mpana zaidi kuhusu mahusiano.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.