-->

Breaking News

Mkwanja aliyolipwa Ceccy kwenye video ya Lil Baby

 Mkwanja aliyolipwa Ceccy kwenye video ya Lil Baby

Mwanamitindo Mtanzania maarufu kwa jina la Ceccу ametokea kama mrembo (video vixen) kwenye video mpya ya wimbo wa rapa wa Marekani, Lil Baby uitwao 'Mrs Trendsetter'.

Ikumbukwe Ceccy aliwahi kufunga ndoa na aliyekuwa mpigapicha wa Wasafi, Lukamba mwaka 2020 na kwa bahati mbaya hawakudumu miaka miwili baadae wakaachana. Baada ya kuachana kila mmoja akawa anafanya shughuli zake lakini Ceccy hakubaki Tanzania akaibukia New York na Miami nchini Marekani.

Tangu atimke nchini Ceccy amekuwa akijishughulisha zaidi na mambo ya uanamitindo na hii inakuwa kazi ya pili kutokea kwenye video ya msanii mkubwa nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ceccy kufanyakazi na mastaa wakubwa nchini humo kwani mwaka 2025 alifanya kazi na Rick Ross kupitia wimbo wa Bags.

Baadhi ya mashabiki wamempongeza mwanadada huyo kwa hatua hiyo kubwa huku wengine wakimtagi aliyekuwa mume wake Lukamba katika posti ya video na kumcheka kuwa amechezea bahati.

Hata hivyo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari nchini Ceccy ameweka wazi namna alivyokutana na Lil Baby mpaka kufanyakazi pamoja na kiasi alicholipwa.

“Namshukuru Mungu haikuwa rahisi kukutana na watu wakubwa kama hawa, Tanzania imeamua kunisapoti kwenye hili toka imeruka hiyo ngoma nimepata meseji na call nyingi.

“Toka nimehamia Miami hii kampuni ambayo nimesaini nayo miezi mitatu iliyopita wao wenyewe ndio walinitumia email wakanambia kwamba natakiwa kushuti music video na Lil Baby na hicho ndio kilitokea. Tegemeeni makubwa Zaidi kuna hiyo na nyingine pia. Nimelipwa dola 12000 (ikiwa ni Zaidi ya Sh 30 million) na hii ndio hela kubwa niliyopokea tangu nianze kufanya kazi ya video vixer,”amesema Ceccy

Mbali na kazi hizo Ceccy pia amewahi kualikwa kwenye hafla ya ugawaji tuzo za Grammy msimu wa 67 pale Crypto.com Arena, Los Angeles Marekani na kwa mujibu wake alisema ndiye Mtanzania pekee aliyealikwa kwenye tuzo hizo.

Ceccy anakuwa mwanamitindo wa pili kutoka Afrika Mashariki kutokea kwenye video za nyimbo za wasanii, awali Lupita Nyongo wa Kenya amewahi kuwa mrembo kwenye video mbalimbali ikiwemo 'Brown Skin Girl' ya Beyonce akimshirikisha Wizkid.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.