-->

Breaking News

Bill Duke atunukiwa Hollywood Walk Of Fame

 Bill Duke atunukiwa Hollywood Walk Of Fame

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Marekani, Bill Duke, ambaye alipata umaarufu kupitia filamu za Predator na Commando, ametunukiwa nyota ya heshima ya Hollywood Walk of Fame.

Hafla hiyo ilifanyika siku chache zailizopota ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa katika 6201 Hollywood Boulevard, Los Angeles, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu kwa zaidi ya miongo mitano.

Ametunukiwa nyota hiyo katika kitengo cha filamu, kama ishara ya kumpongeza kwa mchango wake wa kipekee, akiwa mbele na nyuma ya kamera.

“Hollywood Chamber of Commerce inajivunia kumkaribisha mwigizaji na mtayarishaji wa filamu maarufu Bill Duke kwenye Walk of Fame wakati wa Mwezi wa Historia ya Watu Weusi kwa mchango wake katika filamu kwa miongo kadhaa,” alisema Ana Martinez, mtayarishaji wa Walk of Fame.

Aidha waandaaji wa tuzo hizo pia wamemtaja Duke kama mbunifu wa kipekee ambaye ameitumikia tasnia ya filamu kwa zaidi ya miongo mitano. Huku akipongeza kwa umahiri wake katika kazi mbalimbali zikiwemo Car Wash, Predator, Commando, Black Lightning, na Get Rich or Die Tryin’, pamoja na kuongoza filamu muhimu kama Deep Cover, A Rage in Harlem, The Killing Floor, na Sister Act 2: Back in the Habit.



Mbali na kazi za filamu, Duke pia ametambulika kwa mchango wake wa kuendelea vipaji kwa vijana wa kizazi kipya akifungua taasisi mbalimbali kama Duke Media, Younite Network, na Duke Media Foundation, The Bill Duke Experience taasisi ambazo zinatoa elimu kwa vyombo vya habari, uelewa wa fedha pamoja na Sanaa ya uigizaji na uandishi.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na mastaa mbalimbali akiwemo Dr Dre, Glynn Turman, Jeff, Nicole Friday wa American Black Film Festival, pamoja na Nathalie Duke, Rais wa Duke Entertainment.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.