-->

Breaking News

Aweka rekodi ya kuvuta gari yenye kilo 991 kwa chuchu

 Aweka rekodi ya kuvuta gari yenye kilo 991 kwa chuchu

Post DesMwanaume mmoja kutoka Finland, maarufu kama The Baron, ameweka rekodi mpya ya dunia baada ya kuvuta gari lenye uzito wa kilogramu 991 kwa kutumia chuchu zake.



Waandaaji wa rekodi za dunia wa Guinness, wamethibitisha hilo ambapo mwanaume huyo alivuta gari la kukokotwa linalofanana na linalotumiwa na farasi.

Taarifa zinaeleza kuwa, jaribio hilo lilihitaji maandalizi ya muda mrefu ya kimwili na kiakili, huku muhusika akieleza uvumilivu wa maumivu na mazoezi kuwa miongoni mwa siri za mafanikio yake.

Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa The Baron kuweka rekodi, kwani Julai 19, 2013 aliwahi kunyanyua uzito wa kilogramu 32.6 kwa kutumia chuchu zake.



Rekodi hiyo imeendelea kuvuta hisia za wengi, ikionesha namna uwezo wa mwili wa binadamu unavyoweza kufikia viwango vinavyoonekana kuwa vigumu au visivyowezekana.criptions

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.