Salman Khan Na Shah Rukh Khan Hawana Urafiki Wa Kweli

Mwandishi maarufu wa filamu za Bollywood na baba mzazi wa Salman Khan, Salim Khan, ameweka wazi kuwa mwanaye na mwigizaji Shah Rukh Khan hawana urafiki wowote, badala yake wanaheshimiana tu.
Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni ameeleza ingawa mastaa hao wanaheshimiana katika masuala ya kazi lakini ukweli ni kuwa hakuna urafiki wa kweli baina yao.
“Watu wote wanaongea kuhusu vita kati ya Shah Rukh Khan na Salman Khan… Kwani ni marafiki? Je, washindani wanaweza kuwa marafiki?, Kwanini wasiwe marafiki ili kutengeneza nguvu pamoja?
.
“Je, inawezekana kuwa na urafiki kati ya washindani, niwaambie tu haiwezekani kuwa na upendo wa dhati kati ya washindani wawili ambao wanafanya kitu kinachofanana,”amesema Salim Khan.
Aidha ameongeza kuwa ingawa mastaa hao wawili wanaweza kuheshimiana, lakini asili ya kazi yao inawaweka katika ushindani wa kudumu na haoni kama watakuja kuwa marafiki wa dhati. Huku akiongezea kuwa hiyo ni hali ya kawaida katika tasnia ya filamu.
Utakumbuka wawili hao wamefanya kazi za pamoja ikiwemo Karan Arjun (1995), Hum Tumhare Hain Sanam (2002), Dushman Duniya Ka, Har Dil Jo Pyar Karega. Nyingine ni Kuch Kuch Hota Hai, Om Shanti Om, Tubelight (2017) na Zero (2018)
Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni ameeleza ingawa mastaa hao wanaheshimiana katika masuala ya kazi lakini ukweli ni kuwa hakuna urafiki wa kweli baina yao.
“Watu wote wanaongea kuhusu vita kati ya Shah Rukh Khan na Salman Khan… Kwani ni marafiki? Je, washindani wanaweza kuwa marafiki?, Kwanini wasiwe marafiki ili kutengeneza nguvu pamoja?
.“Je, inawezekana kuwa na urafiki kati ya washindani, niwaambie tu haiwezekani kuwa na upendo wa dhati kati ya washindani wawili ambao wanafanya kitu kinachofanana,”amesema Salim Khan.
Aidha ameongeza kuwa ingawa mastaa hao wawili wanaweza kuheshimiana, lakini asili ya kazi yao inawaweka katika ushindani wa kudumu na haoni kama watakuja kuwa marafiki wa dhati. Huku akiongezea kuwa hiyo ni hali ya kawaida katika tasnia ya filamu.
Utakumbuka wawili hao wamefanya kazi za pamoja ikiwemo Karan Arjun (1995), Hum Tumhare Hain Sanam (2002), Dushman Duniya Ka, Har Dil Jo Pyar Karega. Nyingine ni Kuch Kuch Hota Hai, Om Shanti Om, Tubelight (2017) na Zero (2018)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.