Usher afunguka kuzichapa na Justin Bieber

Mwimbaji wa RnB kutokea Marekani, Usher Raymond IV (47), amekanusha vikali madai kwamba alipigana au kubishana na msanii mwenzake, Justin Bieber (32), kwenye sherehe ya Oscars iliyoandaliwa na Beyonce na Jay Z.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita TMZ kuripoti kwamba wawili hao waliingia katika ugomvi mkubwa baada ya Usher kumfuata Bieber akiwa na hasira kwenye sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mastaa wengi.
Hata hivyo, rafiki wa Usher, rapa Da Brat akizungumza kwa niaba yake kwenye kipindi cha The Rickey Smiley Show, amesema kuwa Usher alimwambia ripoti hiyo ilikuwa imetiwa chumvi kwa maneno ya uongo!.
"Nimezungumza na Usher, na alisema, 'Hii ripoti imezidishwa chumvi kuhusu mazungumzo yaliyotokea," alisema Da Brat na kuongeza. "Usher amekuwa akimuunga mkono Justin Bieber katika mambo mengi kwa miaka mingi, na hilo linaweza kuthibitishwa."
"Bieber yuko kwenye safari yake mwenyewe, akikabiliana na hali yake binafsi aliyojitengenezea. Usher anamtakia mema tu, na hawana uhasama wowote kuna upendo mkubwa kati yao,” alieleza.
"Watu wanapenda kutoa mambo nje ya muktadha wanapoona kitu na kukikuza zaidi. Niko hapa kusema hakuna tatizo kati yao. Wako sawa kabisa na wanaheshimiana na kila mmoja anamuunga mkono mwenzake," amesema Da Brat

Kwa mujibu wa vyanzo vya TMZ, ingawa mabishano hayo hayakufikia hatua ya kupigana, yalikuwa makali. Chanzo kimoja kilidai kwamba Bieber amekuwa na tabia ya ukorofi kwa Usher, na anajaribu kuwaondoa watu wote waliokuwa sehemu ya maisha yake ya awali.
Utakumbuka mwimbaji huyo pamoja na meneja wake wa zamani, Scooter Braun, walikuwa watu muhimu katika hatua za mwanzo za mafanikio ya Bieber, huku Usher akiwa kama mlezi wake kwa muda mrefu.
Alimsaidia Bieber kupata umaarufu duniani kote akiwa na umri wa miaka 13 tu baada ya kipaji chake kugunduliwa na Scooter Braun. Na punde tu Usher na Bieber waliimba pamoja wimbo, Somebody to Love (2010).
Licha ya sapoti hiyo, mnamo Februari 2024, vyanzo vilieleza wamba Usher alimwomba Bieber kushiriki katika onyesho lake la mapumziko la Super Bowl, lakini Bieber alitupilia mbali ombi hilo.
Badala yake, Usher aliwaleta jukwaani mastaa wengine kama Alicia Keys na H.E.R na kuweza kutumbuiza pamoja na bendi, huku ripoti zilizodai kuwa Bieber angetumbuiza naye zikibaki kama tetesi tu.
Mwaka 2016, Usher alipokuwa akizungumzia changamoto za kisheria zilizokuwa zikimkabili Bieber, alisema msanii huyo ni kama mtoto wake na amekuwa akipokea ushauri wake.
"Kama mlezi, amekuwa akikubali maoni yangu, naweza kumpa mtazamo wangu. Ni kama mtoto kwangu, hivyo sioni kama biashara. Ni kama nazungumza na mtu aliyepitia magumu," alisema Usher kwenye kipindi cha The Howard Stern Show.
Hata hivyo, Bieber kupitia Instagram alitema nyongo kuhusu maisha aliyopitia awali akisema yamemuachia majereha kutokana wasimamizi wake walijali zaidi kipaji chake kuliko utu wake!.
"Nililelewa katika mfumo uliothamini kipaji changu lakini haukulinda utu wangu kila wakati. Kulikuwa na nyakati nilihisi kutumika, kuharakishwa, na kubadilishwa kuwa kitu ambacho sikuchagua shinikizo hili limeacha majeraha yasiyoonekana jukwaani," alieleza Bieber.
Justin Bieber alivuma duniani na albamu yake ya kwanza, My World 2.0 (2010) iliyoshika namba moja Billboard 200 na kumfanya kuwa msanii mdogo zaidi kuongoza chati hizo baada ya miaka 47. Albamu hiyo ndio iliyotoa wimbo wake maarufu 'Baby' akimshirikisha Ludacris.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.