Mkali wa Hip Hop kutoka Marekani Young Thug ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 5 jela amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuachia wimbo mpya ambao ni kwa ajili ya kuwaomba radhi mastaa wenzake akiwemo Drake.
Katika wimbo huo uitwao ‘Man I Miss My Dogs’, Thug anasikika akiimba kwa sauti ya upole na unyenyekevu huku akiwaomba msamaha wasanii wenzake akiwemo Drake, 21 Savage, Lil Baby pamoja na mpenzi wake Mariah the Scientist.
Thug ameachiwa wimbo huo baada ya mazungumzo yake wakati yupo gerezani kuvujishwa mitandaoni ambapo alisikika akiwazungumzia vibaya mastaa hao.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Thug kuomba msamaha hadhari kupitia wimbo ambapo alianza na mpenzi wake Mariah, akisema hofu yake kubwa ni kumpoteza kutokan ana maneno mitandaoni, pia alimtaja Drake kama kaka yake na kumshukuru kwa kumsapoti katika kazi zake za muziki huku akiadi kutomdiss tena.
Kwa upande 21 Savage amemtaka aendelea kumsaidia na kuacha kusikiliza maneno ya watu kwani yatawaweka mbali, vilevile amemuomba GloRilla msamaha kwa kumuita mbaya huku akidai kuwa anajutia sana kutoa kauli kama hizo.
Utakumbuka kuwa maneno hayo Young Thug aliyatamka wakati yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka 5 jela kwa makosa ya uhalifu wa mtandao wa magenge, dawa za kulevya na kumiliki silaha. Hata hivyo aliachiwa huru kutoka gerezani Oktoba 31,2024, baada ya kukiri mashtaka (plea deal) katika kesi ya RIC.