A Zeno.FM Station Siyo Usaliti Ni Nguvu Ya Pesa

Siyo Usaliti Ni Nguvu Ya Pesa

IDDY AMAN
0

 Siyo Usaliti Ni Nguvu Ya Pesa

Kumekuwa na mashambulizi mengi ya maneno ya kashfa na pongezi huko mitandaoni na nje ya mitandao, kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakiitwa kwenda kutoa burudani kwenye matamasha ya Simba Day na Yanga Day.

Maneno hayo wanaambiwa kwa kuonekana wasaliti na wengine kuonekana hawana msimamo. Kwasababu ya kujitangaza kushabikia timu fulani na baada ya hapo kwenda kutoa burudani kwenye timu pinzani. Na bado wakipanda jukwaani wanainadi timu pinzani kwa kutoa madongo yenye kuwaudhi mashabiki wa timu hizo na kuanza kuwarushia maneno.

Hii ya kutoa burudani inaweza ikawa wasanii hawa wanamaanisha muziki ni biashara kwa kutegemea muziki katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hii ya kushambuliwa wasanii haijaanza leo wala jana, ni muda mrefu na imewahi kutokea kwa wale ambao wamewahi kutoa burudani kwenye majukwaa ya Simba Day na Wiki ya Mwananchi ambao ni Alikiba, Diamond Platnumz, Marioo, Meja Kunta, Dulla Makabila, Mbosso, Zuchu na wengine wengi. Ni wamejiongeza na kufanya biashara na wamejikuta wakipiga pesa za maana tu.

Katika makala hii itawaorodhesha wachache waliochukua uamuzi huo na kujikuta wakishambuliwa
Diamond Platnumz
Huyu mwaka 2020 aliwahi kujitangaza kuwa ni shabiki wa Simba, aliingia studio na kutoa wimbo 'Simba', lakini mwaka 2023 akaja kutumbuiza tamasha la Yanga Day hapo ndipo alipoanza kupata mashambulizi ya maneno kuwa ni msaliti na wengi kumwambia hana msimamo na timu yake anayoishabikia.

Alikiba
Mwanzo alifahamika ni shabiki wa timu ya Yanga, lakini mwaka 2024 alipanda jukwaa la Simba Day kutumbiza na alitunga wimbo wa 'Mnyama' ambao unaendelea kufanya vizuri hadi sasa.

Msaga Sumu
Aliwahi kuwa shabiki wa Simba, na baadae akawa shabiki wa Yanga. Niguli wa muziki wa singeli, aliwahi kutunga wimbo 'Naipenda Simba' mwaka 2022 kwa ajili ya Simba Day, na ulifanya vizuri, mwaka 2023 akatoa wimbo wa 'Watoto wa Jangwani' na kutumbuiza katika yanga Day. Hapo alishambuliwa kwa kuambiwa ni msaliti

Dulla Makabila
Kwake ni kama amezoea kushambuliwa na mashabiki wa Simba na Yangaz kwani
Mwaka 2020 alipanda jukwaani la Yanga Day kutumbuiza, mwaka 2021 alipanda jukwaa la Simba day kutumbuiza, lakini pia amekuwa ni mtu wa kutoa nyimbo za Simba na Yanga kitu ambacho mashabiki zake hawamuelewi, mwaka Jana akatunga wimbo wa Simba akashambuliwa sana hadi kukataliwa kutotumbuiza kwenye jukwaa la Simba, ndipo akatunga wimbo wa Yanga kwa wakati huo.

Zuchu
Ni shabiki wa Simba mwaka huu 2025 ametangazwa kutumbuiza Yanga Day, Toka hapo huko mitandaoni anashambuliwa na mashabiki ya simba kuwa ni msaliti kwani mwaka 2022 alitumbuiza Simba day.

Mbosso
Ni shabiki wa timu ya Simba, Juni 2025, alitumbuiza jukwaa la Yanga walipo kuwa wana shekerekea kilele cha paredi cha mataji matano ikiwa ni hitumisho la mafao kwa timu hao, hivi karibu msemaji wa klabu ya Simba, Ahmed Ally aliweka wazi Mbosso atakuwa jukwaani kuwapa burudani mashabiki wa klabu hiyo kwenye tamasha la Simba Day.

Marioo
Mwanzo alijitangaza kuwa ni shabiki wa timu ya Simba, mwaka 2021 alipanda jukwaa la Simba Day kutumbuiza, mwaka 2022 alipanda jukwaa la Yanga Day kutumbuiza, hii kwa mashabiki wa Simba kumshambulia na kusema ni hana msimamo.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default