Leo, Septemba 13, 2025, dunia inaadhimisha miaka 29 tangu kifo cha rapa nguli wa Marekani, Tupac Amaru Shakur, aliyeuawa kwa risasi jijini Las Vegas mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25.
Tupac, ambaye alijulikana kwa jina la "2Pac," alitumia muziki wake kuzungumzia changamoto za kijamii ikiwemo ubaguzi, umasikini na vurugu mitaani. Albamu zake kama All Eyez on Me na Me Against the World bado zinaendelea kufanya vizuri katika historia ya muziki wa hip hop.
Licha ya kufariki mapema, jina lake limeendelea kuishi huku likitoa taswira mpya kwa wasanii wa kizazi kipya. Aidha licha ya kufariki kifo chake bado kimeibua gumzo huku wengine wakiamini kwamba anaweza kuwa hai hadi leo.

Utakumbuka, Tupac Shakur alizaliwa 16 Juni 1971 jijini New York, Marekani, na alifariki Septemba 13,1996 Las Vegas kwa kupigwa na risasi.
Alishambuliwa kwa risasi usiku wa Septemba 7, 1996 jijini Las Vegas, alikimbizwa hospitali ya University Medical Center (UMC) ambako alilazwa hospitalini hapo kwa siku 6, kisha akafariki dunia Septemba 13, 1996 kutokana na majeraha makubwa ya risasi kwenye mapafu na viungo vya ndani.
Baada ya kifo cha Tupac Shakur mwaka 1996, majina kadhaa ya mastaa na wanachama wa magenge walihusishwa akiwemo aliyekuwa bosi wa Death Row Records, Suge Knight, Orlando Anderson (Baby Lane), Keefe D (Duane Keith Davis), Biggie Smalls (The Notorious B.I.G.) pamoja na Diddy lakini hakuna ushahidi mpaka sasa unaothibisha kuhusika katika tukio hilo.