A Zeno.FM Station Misri Ukiua Paka Unahukumiwa Kifo

Misri Ukiua Paka Unahukumiwa Kifo

IDDY AMAN
0

 Misri Ukiua Paka Unahukumiwa Kifo

Katika Misri ya kale paka walihesabiwa kuwa viumbe wa thamani ya kipekee ambapo Wamisri waliamini paka walihusiana na Mungu ‘Bastet’ ambaye alikuwa mlinzi mkuu wa majumbani.

Inaelezwa kuwa huko Bubastis, Paka walipatiwa matunzo zaidi ya yale wanayopewa binadamu na hata wakati ambao paka amekufa basi atazikwa kwa heshima kubwa.

Kwa mujibu wa waandishi wa kale kama Herodotus, kuua paka ilikuwa kosa kubwa mno. Hata kama kosa lilitokea kwa bahati mbaya, jamii ingeweza kumshambulia mhusika huku ambaye angepatikana hatia angeweza kuhukumiwa adhabu ya kifo.

Aidha moja ya ushahidi mkubwa ni kisa maarufu kilitokea mwaka 525 KK kwenye vita vya Pelusium, ambapo jeshi la Wapersia walitumia paka na wanyama wengine kama kinga ambapo Askari wa Misri walihofia kuwadhuru wanyama hao, jambo ambalo lilichangia kushindwa kwa vita.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default