A Zeno.FM Station SIMBA SC YAFANYA KIKAO KIZITO KABLA YA KUIVAA YANGA JUMANNE

SIMBA SC YAFANYA KIKAO KIZITO KABLA YA KUIVAA YANGA JUMANNE

IDDY AMAN
0

 

UONGOZI wa klabu ya Simba leo umekutana na wachezaji na benchi la Ufundi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumanne kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Ally Mangungu kwa pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Wakurugenzi, Crestentius John Magori.
Kikao hicho kinafanyika siku tatu baada ya tamasha la Simba Day, klabu ikitambulisha kikosi chake kamili cha msimu mpya na kucheza mechi ya kirafiki dhidi y Gor Mahia ya Kenya ambayo walishinda 2-0.
Taarifa ya Simba juu ya kikao hicho imesema ni kupanga mikakati ya msimu ambao watauanza Jumanne kwa mchezo dhidi ya Yanga.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default