A Zeno.FM Station Tiwa Savage Azua Mazito

Tiwa Savage Azua Mazito

 Tiwa Savage Azua Mazito


Mwanamuziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuzungumza uhusiano wake wa zamani na staa mwenzake kutoka nchini humo.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake hivi karibuni alifichua kuwa alimjali sana staa huyo lakini alilazimika kuachana naye baada ya kutoonyeshwa heshima na msanii huyo ambaye alimtaka wafanye siri uhusiano wao.

Tiwa alisema kuwa kila walipokuwa kwenye tamasha moja, mpenzi wake huyo alikuwa akivutiwa na wanawake wengine akiwagusa na kuzungumza nao alipomuuliza kuhusu hilo, alipuuzia na kusema anafanya hivyo tu ili watu wasishtukie uhusiano wao.

Aidha kutokana na majibu hayo kumezuka mijadala mbamimbali mitandaoni ambapo baadhi ya mashabiki walidai kuwa staa huyo aliyekuwa akizungumziwa na Tiwa ni msanii Wizkid ambaye hapo awali wawili hao walikuwa karibu sana.

Hata hivyo kutokana na sakata hilo mashabiki wametoa maoni yao mbalimbali huku wakimnanga na kumtolea maneno makali Wizkid wakimtaja kuwa ndio msanii anayeongoza wa kuwa na kiburi pamoja na dharau.

Mpaka kufikia sasa Wizkid hajajibu tuhuma hizo, vile vile kwa upande wa Tiwa naye hatajotea ufafanuzi kuhusiana na sataka hilo kama mtu aliyekuwa akimzungumzia ni Wizkid.
Tags :-

Post a Comment

0 Comments