Mwanamuziki wa Bongo Fleva Yammy, hivi karibuni amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuacha kitovu chake wazi akiingilia maduka ya Mlimani City.
Ilikuwa majira ya jioni, Yammy ambaye anatamba na nyimbo kama 'Kukupenda' 'Tunapendezana' 'Raha' na nyingine nyingi, alishuka kwenye gari na kwenda dukani ndipo baadhi ya watu wakajaa kumwangalia huku wengi wakizungumzia kitovu chake alichokiacha nje siyo jambo sahihi akiwa maneno ambayo siyo ya shughuli za muziki.
Tukio hilo ambalo limeshuhudiwa na Mwanaspoti, lilichukua dakika saba, wapo watu waliokuwa wanafurahia mwonekano wake kwa kumuona 'Live' na wengine kumsogelea kwa kutaka kumgusa ila ilishindikana kutokana na Yammy kuongozana na na wanaume wawili ambao hawakufahamika majina.
"Ila wasanii bwana, hivi hawawezi kujistiri mavazi yao wakiwa nje ya kazi zao za muziki? Yaani kama huyu Yammy amevaa kama anaenda kwenye shoo wakati amekuja kwa mahitaji mengine kabisa," alisema kaka mmoja aliyetambulika wa jina la Sudy.
"Sasa huyu Yammy anaona raha hapa watu walivyojaa kumutazama hicho kitovu chake? Mbona binti mdogo anashindwa kuvaa vizuri, sehemu zingine anavamiwa huyu na watu wenye nia mbaya," alisema mama mmoja aliyejitambulisha jina la mama Mboni.
Aidha Mwanaspoti, lilibahatika kuongea na Yammy, kuhusu watu kujikusanya kumwangalia na alisema ni kawaida kwa msanii.

"Mimi sio tatizo watu kunitazama, mimi ni msanii na sababu pia huwa sijichanganyi sana na watu, hivyo wapo ambao wananishangaa kwa mazuri na mabaya, ila kuhusu kuachia kitovu hii ni stali yangu tu naipenda watu wasinihukumu mbona huwa navaa sana mavazi ya stara, tena haya ni kwa mara nyingi, sema pale nilikuwa naenda kushooting nikapitia mara moja Mlimani City," alisema.