A Zeno.FM Station Mapacha Wa Diddy Wanajambo Lao

Mapacha Wa Diddy Wanajambo Lao

 Mapacha Wa Diddy Wanajambo Lao


Licha ya baba yao kuwa gerezani huku akisubiria hukumu yake, watoto wa nguli wa Hip Hop kutoka Marekani Diddy, Jessie na D’Lila wamepanga kuonekana kwa mara ya kwanza katika jukwaa la mitindo litakalofanyika jijini New York.

Kwa mujibu wa TMZ mapacha hao wamepanga kufunga Wiki ya Mitindo jijini huo ikiwa ni muonekano wao wa kwanza kuufanya wakiwa chini ya chapa yao iitwayo ‘12TWINTY1’ ambayo waliizindua mwanzoni mwaka mwaka huu wakisaidiwa na mwanamitindo Kimora Simmons.

Katika onyesho lao la awali kwenye jukwaa la mitindo la NYFW walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi ya rangi ya zambarau, Onyesho ambalo lilifanyika kwenye jumba la Avalon Hollywood huko Los Angeles Septemba 4, 2025.

Wiki ya Mitindo ya New York (NYFW) ni tukio muhimu katika ulimwengu wa mitindo, ambapo wabunifu na wanamitindo kutoka sehemu mbalimbali za dunia huonyesha kazi zao.

Aidha kuhusu kutofanya vizuri kwa sababu ya baba yao, mapacha hao wamefunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa baba yao yupo kwenye mood nzuri, moyo wake uko poa na kwamba kila kitu kitakwenda sawa kama ambavyo kilipangwa.
Tags :-

Post a Comment

0 Comments