Kufungwa hakumpendezi mtu na maumivu ya kufungwa hayazoeleki, hasa ukifungwa na mpinzani wako mkuu, na ukifungwa na mpinzani mmoja mara nyingi
Lakini kwa mechi ya leo tunakila sababu ya kujivunia timu yetu na kuwapongeza Wachezaji wetu kwa ubora mkubwa walionesha
Kwa muda mrefu hatujacheza mechi kwa kiwango kikubwa namna hii
Dakika 45 za kipindi cha kwanza peke yake zingetosha kurejesha heshima yetu ila bahati haikuwa kwetu
Pamoja na kupoteza mchezo wa leo lakini umetupa taswira tutakua na msimu wa aina gani huko mbeleni.
Itoshe kusema tuu tutakua na msimu bora sana kulingana na kikosi tulichokua nacho
Jicho lenye machozi halioni mbali hivyo mnaweza msinielewe hii leo, lakini tuishi humu Wana Simba safari hii timu tunayo na tutafanikiwa sana Insha Allah
Tumefanya usajili bora sana, Wachezaji wetu wapya wameonesha viwango vya hali ya juu
Niwaombe ndugu zangu Wana Simba tutulie na tujipange kuanza msimu kwa kishindo, kilichopotea ni kidogo sana kulinganisha na vikubwa ambavyo viko mbele yetu
Ameandika Ahmedy Ally Msemaji wa Simbasc