CHANZO CHA PICHAGETTY IMAGES
Bayern Munich wamempiga bei kiungo wa kati wa Ufaransa Michael Olise mwenye umri wa miaka 23 kwa pauni milioni 100 huku Liverpool na vilabu vingine vikubwa vya Ulaya vikiwa na nia ya kutaka. kumnunua (Football Insider)
Chelsea wanatafuta kumsajili beki wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi, 25, na kipa wa AC Milan na Ufaransa Mike Maignan, 30, kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao. (TBR Football)
Manchester City hawana uwezekano wa kumwongezea mkataba kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, na hivyo kufungua njia kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuondoka kwa uhamisho wa bil amalipo msimu ujao, huku Juventus na Benfica zikionyesha nia. (AS - In Spanish)

Liverpool, Arsenal na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Ayyoub Bouaddi, 17. (TeamTalks}
Bayern Munich wanatazamia kumnunua winga wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 23 Nico Williams msimu ujao. (Fichajes - In Spanish)
Chelsea itakabiliana na ushindani kutoka kwa Bayern Munich katika kumsaka winga wa Lyon na Ubelgiji Malick Fofana, 20. (Caught Offside, via Christian Falk).
Beki wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 Mfaransa Ibrahima Konate ameamua kutoongeza mkataba wake Anfield na atasaini Real Madrid msimu ujao wa joto. (Fichajes - In Spanish)

Manchester United bado wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Brighton na Cameroon Carlos Baleba baada ya kumkosa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 msimu huu. (Football Insider)
Winga wa Manchester United Sam Mather, 21, atatafuta kuondoka Old Trafford mwezi Januari baada ya siku ya makataa ya kuhamia Kayserispor kupita. (Manchester Evening News)
Chelsea imetuma maskauti kumtazama mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 20 na Uturuki Kenan Yildiz. (Offside trap)