AZAM FC YAIFUATA AL MERREIKH JUBA MAPEMA MECHI JUMAMOSI IJAYO - IDDYNATION SITE

Breaking News

AZAM FC YAIFUATA AL MERREIKH JUBA MAPEMA MECHI JUMAMOSI IJAYO

 

KIKOSI cha Azam FC kimeondoka Alfajiri ya leo kwenda Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Al Merreikh FC, maarufu kama Al Merreikh Juba Jumamosi ya wiki ijayo, Septemba 20 Uwanja wa Juba Jijini Juba.
Timu hizo zitarudiana Septemba 28 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya AS Port ya Djibouti na KMKM ya Zanzibar.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.