A Zeno.FM Station Hatimaye Joti afichua siri ya kambi

Hatimaye Joti afichua siri ya kambi

 Hatimaye Joti afichua siri ya kambi



Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhavile ‘Joti’, amesema anapokuwa lokesheni kwa ajili ya kazi zake anaweza kuzinguana na yeyote kama hawafahamiani endapo ataleta utani.

Joti ambaye aliwahi kutesa na kikundi cha vichekesho cha Ze Komedi na Orijino Komedi, aliliambia Mwananchi huwa anakuwa mtu mwingine kabisa na hata moyo wake unakuwa mgumu kwa sababu kwenye kazi huwa hatanii, ni kazi kazi.

Alisema wasanii wanapokuwa lokesheni, mambo mengi hutokea ikiwemo kutaniana lakini kwake ingawa ni mchekeshaji na mpenda utani lakini si lokesheni.

“Unajua ninapokuwa lokesheni ndiyo nakuwa natengeneza mkate wangu, sasa mtu anaponiletea utani kwenye mkate wangu hapo hatuwezi kuelewana na ukweli lokesheni huwa sihitaji masihara kabisa,” alisema Joti ambaye amejizolea umaarufu pia kutokana na kazi zake za mitandaoni hasa YouTube na kubeba tuzo kadhaa zinazomdhihirisha ni mmoja wa wachekeshaji wakubwa zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.
Tags :-

Post a Comment

0 Comments