
Jeshi la Polisi: Marufuku Kuja na Silaa Dabi ya Kariakoo Leo Kwa Mkapa
Kuelekea mchezo wa soka wa Dabi ya Kariakoo kati ya klabu ya Yanga Sc dhidi ya Simba Sc utakaofanyika kesho Juni 25, 2025, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limechukua tahadhali zote za kiusalama kwa kuwa inaonesha mchezo huo utakuwa na mkusanyiko mkubwa wa wapenzi wa soka kutoka maeneo ya ndani na nje ya Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Jumanne Muliro amesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufika uwanjani na silaha ya aina yoyote isipokuwa baadhi ya askari wenye jukumu la usalama eneo hilo Na kubainisha kuwa magari yatakayo ruhusiwa kuingia uwanjani ni yale yenye kibali maalum.
“Jeshi la Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wapenda soka wote kujiepusha na vitendo visivyo vya kiungwana kabla, wakati na baada ya mchezo huo,”—amesema Kamanda Muliro.