A Zeno.FM Station Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Nunez kujiunga na Napoli iwapo ataondoka Liverpool

Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Nunez kujiunga na Napoli iwapo ataondoka Liverpool

IDDY AMAN
0



.

Chanzo cha picha,Reuters

Maelezo ya picha,David Nunez

Mshambulizi wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 25, ameifanya Napoli kuwa mahali anapopendelea zaidi ikiwa ataondoka Anfield msimu huu wa joto. (Soccer Italia)

Nottingham Forest imekataa ofa kutoka kwa Newcastle yenye thamani ya pauni milioni 45 kwa winga wa Uswidi Anthony Elanga, 23, ambaye thamani yake ni pauni milioni 60. (Sky Sports),

Chelsea wana matumaini ya kukamilisha haraka mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jamie Gittens, huku Bayern Munich pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Subscription Required)

Barcelona wanafikiria kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27. (Guradian)

Newcastle wako tayari kumfanya mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia nia ya Liverpool, Barcelona na Arsenal. (Times – Subscription Required)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Alexander Isak

Fenerbahce wanavutiwa na winga wa Manchester United mwenye umri wa miaka 25 Muingereza Jadon Sancho, ambaye thamani yake ni pauni milioni 25. (Sportsport)

Sunderland wameiuliza Sassuolo kuhusu kupatikana kwa winga wa Ufaransa Armand Lauriente, 26. (ESPN)

Everton na Manchester United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Leicester na Nigeria Wilfred Ndidi, 28, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 9 katika mkataba wake. (Sportsport)

Nottingham Forest na Marseille wanavutiwa na kiungo wa kati wa Ajax na Uingereza Jordan Henderson, 35, ambaye ana kipengele katika mkataba wake kitakachomruhusu kuhama kwa uhamisho huru. (Mail)

Leeds bado hawajapokea ofa kwa mlinda lango wa Ufaransa Illan Meslier, 25, licha ya ripoti kuwa anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Fenerbahce. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nico Williams

Kipa wa Chelsea Muhispania Kepa Arrizabalaga, 30, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Arsenal kwa mkataba wa pauni milioni 5 wiki hii. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Athletic Bilbao raia wa Uhispania Nico Williams, 22, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 50 katika kandarasi yake, ameiambia klabu hiyo kuwa anakusudia kusaini na klabu ya Barcelona. (Athletic – Subscription Required)

Everton, Brentford, West Ham na Fulham wanafikiria kumnunua winga wa Ipswich mwenye umri wa miaka 21 wa Uingereza Omari Hutchinson. (Mail)

Crystal Palace bado inaweza kuzuiwa kucheza Ulaya msimu ujao licha ya John Textor kuuza hisa zake 43% ili kujaribu kufuata sheria za Uefa za umiliki wa vilabu vingi. (Times – Subscription Required), nje

Burnley wanatayarisha dau la pauni milioni 12 kumnunua mshambuliaji wa Lazio wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, Loum Tchaouna, mwenye umri wa miaka 21. (Soccer Italia)

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default