-->

Breaking News

Wiz Khalifa Kwenye Orodha ya Wanaotafutwa Romania

Wiz Khalifa Awekewa Waraka wa Kutafutwa Romania Baada ya Kesi ya Bangi

Rapa maarufu wa Marekani Wiz Khalifa amewekwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa nchini Romania baada ya kushindwa kufika kwa ajili ya kutumikia kifungo cha miezi tisa jela kufuatia kesi ya kupatikana na bangi mwaka 2024.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kimataifa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya mahakama kuthibitisha hukumu dhidi ya msanii huyo anayefahamika kwa kuzungumzia matumizi ya bangi katika muziki na maisha yake binafsi.

Sakata hilo lilianza wakati wa tamasha la muziki la Beach Please Festival lililofanyika katika eneo la pwani ya Black Sea mwaka 2024, ambapo Wiz Khalifa alidaiwa kuvuta bangi akiwa jukwaani mbele ya mashabiki.

Baada ya maonesho hayo, polisi walidai kumkuta akiwa na gramu 18 za bangi, jambo lililopelekea kufunguliwa kwa kesi dhidi yake.

Mahakama ya Constanța Court of Appeal mwezi Februari 2026 ilitupilia mbali rufaa yake ya kuomba kusimamishwa kwa adhabu hiyo, hatua iliyofanya hukumu yake kuwa ya mwisho na rasmi.

Ripoti zinaeleza kuwa kuwekwa kwake kwenye orodha ya wanaotafutwa kunaweza kuipa Romania nafasi ya kuomba akamatwe katika mataifa mengine ya Ulaya kupitia mfumo wa European Arrest Warrant iwapo atasafiri ndani ya bara hilo.


Baada ya tukio hilo mwaka 2024, Wiz Khalifa aliomba radhi kupitia mitandao ya kijamii akisema hakumaanisha kuidharau Romania kwa kuvuta bangi akiwa jukwaani.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za burudani, Hip Hop na mastaa wa kimataifa.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.