-->

Breaking News

Samia akutana na Didier Drogba, amuomba awe balozi AFCON 2027

Samia akutana na Didier Drogba, amuomba awe balozi AFCON 2027

Samia akutana na Drogba, amuomba awe balozi AFCON 2027


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea FC, Didier Drogba, katika Ikulu ya Chamwino leo Mei 5, 2026.

Katika mazungumzo hayo, Rais Samia amemuomba nyota huyo kuwa balozi wa Tanzania kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, hatua inayolenga kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia soka.

Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Drogba ili kubadilishana uzoefu katika kuanzisha na kuendesha vituo vya kukuza vipaji (sports academies).

Kwa upande wake, Drogba amemshukuru Rais Samia kwa mwaliko huo na kuonesha utayari wake wa kushirikiana na Tanzania katika kukuza michezo na vipaji vya vijana.

Mbali na mafanikio yake uwanjani, Drogba anatambulika pia kwa mchango wake wa kijamii, ikiwemo kusaidia kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Ivory Coast mwaka 2005.

Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo nchini kuelekea AFCON 2027.






No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.