Priscilla Ojo afunguka: Tulipanga kupata watoto 16 na Jux, sasa mambo yamebadilika
Mke wa msanii wa Bongo Fleva, Jux, Priscilla Ojo, amesema kuwa awali walikuwa na mpango wa kupata watoto 16 walipoanza uhusiano wao, lakini sasa wamebadili mawazo baada ya kupata mtoto wao wa kwanza.
Priscilla, raia wa Nigeria, amefunguka hayo katika mahojiano yake na Chude Jideonwo, akieleza kuwa mipango yao imebadilika kutokana na uzoefu wa uzazi.
“Nilipokutana na mume wangu, tulisema tutakuwa na watoto 16, lakini sasa baada ya kupata mtoto mmoja, mpango unabadilika,” alisema Priscilla.
Ikumbukwe kuwa wawili hao walitangaza ujauzito Julai 24, 2025 kupitia Instagram, na baadaye Agosti 2025 wakabarikiwa kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Rakeem.
Mtoto huyo alizaliwa nchini Canada na ana uraia wa nchi hiyo.
Habari hii imeibua mjadala mkubwa mitandaoni huku mashabiki wakishangazwa na idadi kubwa ya watoto waliokuwa wamepanga hapo awali.




No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.