-->

Breaking News

Salman Khan Asema Anataka Mtoto Lakini Sio Ndoa

Salman Khan Afunguka Kutamani Mtoto, Awashukia Paparazzi Hospitalini

Muigizaji mkongwe wa Bollywood, Salman Khan, ameendelea kuwa gumzo baada ya kufunguka kuhusu maisha yake binafsi na kueleza kuwa licha ya kutokuwa na mpango wa kuoa, bado anatamani siku moja kuwa baba.

Katika mahojiano yake ya awali, Salman alisema aliwahi kuwa na mpango wa kupata mtoto lakini alikumbana na changamoto za sheria nchini India ambazo zinahitaji mtu kuwa kwenye ndoa ili kukidhi baadhi ya taratibu za kupata mtoto.

“Nilikuwa na mpango huo. Ulikuwa mpango wa kupata mtoto, si wa kupata mke. Lakini kwa mujibu wa sheria za India hilo haliwezekani. Sasa tutaona nini cha kufanya,” alisema Salman Khan.

Muigizaji huyo pia alisisitiza kuwa anapenda sana watoto, ingawa suala la ndoa bado halipo kwenye mipango yake ya haraka.

Mbali na hilo, Salman amekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya video kusambaa ikimuonesha akibishana na paparazzi nje ya hospitali alipokwenda kumtembelea mgonjwa.

Katika tukio hilo, Salman alionekana kukasirishwa na wapiga picha waliokuwa wakimfuatilia huku wakipiga kelele katika mazingira ya hospitali.

Baadhi ya mashabiki walionesha kumuunga mkono huku wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu faragha ya watu hasa wanapokuwa kwenye mazingira nyeti kama hospitali.


Baada ya tukio hilo, Salman Khan alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa ujumbe mkali kuhusu umuhimu wa kuheshimu maisha binafsi ya watu kuliko kutanguliza habari za burudani.

“Kweli picha ni muhimu au maisha?” alihoji Salman katika ujumbe wake uliosambaa kwa kasi mitandaoni.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za Bollywood, burudani za kimataifa na mastaa duniani.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.