Mr Blue Alivyotaka Kuacha Muziki na Kutimkia Uingereza
Mr Blue Alivyotaka Kuacha Muziki na Kutimkia Uingereza
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue, amefunguka kuhusu kipindi kigumu maishani mwake kilichomfanya afikirie kuachana kabisa na muziki na kwenda kuanza maisha mapya nchini Uingereza.
Mr Blue amesema mawazo hayo yalikuja baada ya kumpoteza mama yake mzazi, jambo lililomuumiza sana na kumshusha moyo kiasi cha kuona muziki unazidi kumuongezea msongo wa mawazo.
Katika kipindi hicho kigumu, msanii huyo alikuwa tayari amepanga kwenda Uingereza kuwatafuta ndugu wa upande wa baba yake ili kuanza maisha mapya mbali na muziki.
Hata hivyo, akiwa katika hali hiyo alikutana na mtangazaji maarufu B Dozen ambaye alimshauri asiachane na muziki haraka.
Kulingana na Mr Blue, B Dozen alimwambia kama kweli anataka kuacha muziki basi afanye jambo moja la mwisho kwa kurekodi wimbo mmoja kabla ya kufanya uamuzi huo mkubwa.
Mr Blue alikubali ushauri huo na kwenda katika studio za Sai Records ambapo alirekodi wimbo wake maarufu wa “Pesa” mwaka 2024.
Baada ya kurekodiwa, B Dozen alianza kuucheza wimbo huo redioni na kuusambaza kwa wadau mbalimbali wa muziki nchini.
Mwishowe, wimbo huo uligeuka kuwa hit kubwa na kumpatia Mr Blue mafanikio makubwa ikiwemo show nyingi zilizomuingizia fedha za kukamilisha nyumba yake iliyokuwa inahitaji kiasi cha Sh25 milioni.
Simulizi hiyo imeibua hisia kwa mashabiki wengi wa muziki huku wengi wakimsifu B Dozen kwa mchango wake mkubwa katika kuokoa kipaji cha Mr Blue.
Mr Blue ameendelea kuwa mmoja wa wasanii walioweka historia kubwa ndani ya muziki wa Bongo Fleva kupitia nyimbo zake zilizotamba kwa miaka mingi.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za Bongo Fleva, mastaa wa Tanzania na burudani duniani.


No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.