-->

Breaking News

CAF Club Ranking 2026: Mamelodi Sundowns Waongoza Afrika, Simba SC Top 10

CAF Club Ranking 2026: Mamelodi Sundowns Waongoza Afrika, Simba SC Yaingia Top 10

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetoa orodha mpya ya vilabu bora Afrika kwa mwaka 2026 baada ya hatua za nusu fainali za michuano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup.

Orodha hiyo inaongozwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini huku klabu ya Tanzania, Simba SC, ikifanikiwa kuingia kwenye nafasi 10 bora barani Afrika.

Top 10 CAF Club Ranking 2026

Nafasi Klabu Pointi
1 Mamelodi Sundowns 68
2 Al Ahly 66
3 Espérance de Tunis 58
4 RS Berkane 57
5 Zamalek 49
6 FC Pyramids 48
7 USM Alger 47
8 AS FAR 41
9 Al Hilal 39
10 Simba SC 38

Mamelodi Sundowns wameendelea kuthibitisha ubora wao barani Afrika baada ya kufuzu tena fainali ya CAF Champions League huku wakiongoza orodha hiyo kwa pointi 68.

Kwa upande wa Simba SC, kuingia kwenye Top 10 ya Afrika ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ya Tanzania ambayo imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya CAF katika miaka ya hivi karibuni.

Al Ahly ya Misri ambayo ni klabu yenye mataji mengi zaidi ya CAF Champions League imeporomoka hadi nafasi ya pili baada ya kutolewa mapema kwenye michuano ya msimu huu.

Vilabu vya Morocco, Tunisia, Algeria pamoja na Afrika Kusini vinaendelea kutawala orodha hiyo kutokana na mwendelezo wao mzuri kwenye mashindano ya CAF.

CAF Club Ranking hutumika kuonyesha ubora wa vilabu kwa kuzingatia mafanikio yao kwenye mashindano ya kimataifa barani Afrika katika misimu ya hivi karibuni.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za CAF Champions League, Simba SC, Yanga, na soka la Afrika.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.