Usher na Chris Brown wanajambo lao

Kwa miaka mingi mashabiki wa muziki wa R&B wamekuwa wakitamani kuona pambano la kimuziki kati ya Usher na Chris Brown kupitia mfumo wa Verzuz, wakiamini lingekuwa miongoni mwa mapambano makubwa zaidi ya burudani kuwahi kufanyika.
Kwa mujibu wa maoni na mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na tovuti za burudani, mashabiki wanaamini kwamba Usher, ndiye mfalme wa R&B wa miaka ya 2000, na Chris Brown, ndiye mfalme wa R&B wa miaka ya 2010, wote wakiwa na historia kubwa ya nyimbo kali, albamu zenye mafanikio na uwezo mkubwa wa kupagawisha mashabiki wakiwajukwaani.
Hata hivyo, badala ya pambano la live ambalo mashabiki walilitamani, taarifa mpya zinaeleza kuwa wawili hao wameamua kuungana na kufanya ziara ya pamoja iitwayo ‘Raymond & Brown Tour’.
Kupitia mitandao yao ya kijamii wametoa tangazo likionesha kuwa wamepanga kufanya jambo kubwa wakilipa jina la ‘ITS TIME! R&BTOUR #Raymond&Brown’.

Aidha maelezo zaidi kuhusu ziara hiyo bado hayajatolewa. Tangazo hili la ziara ya pamoja linakuja saa chache baada ya Brown kuachia wimbo wake mpya, “Obvious,” ambao uliyopo kwenye album uake ijayo inayotarajiwa kutoka Mei 8,2026.
Kwa mujibu wa maoni ya mashabiki, wanatamani Chris Brown angeanza kupanda jukwaani na Usher angehitimisha usiku huo huku wakimalizia kutumbuiza ngoma ambazo wamezitoa pamoja.
Wawili hao wamewahi kufanya kolabo kadhaa ikiwemo Party (2016) na Back to Sleep (Remix) iliyotoka mwaka 2016.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.